Pata taarifa kuu
BANGUI-CAR

CAR: Raia bado wanaishi kwa hofu licha ya kusimama kwa mapigano

Mwezi mmoja baada ya waasi kuua mamia ya raia kwenye wilaya ya Kaga Bandoro, wakazi wa katikati ya mji huo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, bado wanaishi kwa hofu licha ya uwepo wa vikosi vya walinda amani wa umoja wa Mataifa pamoja na kuendelea kwa zoezi la kunyang'anya silaha.

Gari la wanajeshi wa kulinda amani wa MINUSCA, wakipiga doria jijini Bangui.
Gari la wanajeshi wa kulinda amani wa MINUSCA, wakipiga doria jijini Bangui. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakirejea kwa mara ya kwanza kwenye mji huo, baadhi ya raia waliokimbia wakati wa mapigano, wameonesha kwa vyombo vya habari namna ambavyo mji wao umeharibiwa kutokana na mapigano ambapo watu zaidi ya elfu 8 kwenye mji huo hawana makazi toka kuzuka kwa vurugu nchini humo.

Baadhi ya waliorejea makwao walikutana na magofu yanyumba walizokuwa wakiishi hapo awali, ambapo nyingi zimeharibiwa vibaya kiasi ambacho binadamu hawawezi kuishi.

Octoba 12 mwaka huu, mji huo unaokaliwa na wakristo, ulishambuliwa na wapiganaji waasi wa kiislamu wa Seleka, ambao ndio walioiangusha Serikali ya kitaifa mwezi Machi mwaka 2013.

Katika tukio lililoonekana ni la ulipizaji kisasi dhidi ya kifo cha mwenzao mmoja, wapiganaji hao wa Seleka waliua watu zaidi ya 37, na kuchoma moto kambi ya wakimbizi wa ndani.

watu walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa, waasi hao waliwachoma watu wakiwa hai, alisema Michel Kenze mmoja wa raia walioamua kurejea kwenye mji huo.

Baada ya mashambulizi hayo, miili ya watu waliokufa iliachwa kwenye barabara na kwenye makazi yao, ambapo wanyama pori na mbwa.

Kufuatia mauaji hayo, mamia ya wananchi waliandamana kwenye jiji kuu la nchi hiyo Bangui, wakishinikiza kuondoka nchini humo kwa vikosi vya kulinda amani MINUSCA wakivituhumu kwa kushindwa kutoa usalama wa kutosha kwa raia, kiasi cha kuruhusu makundi ya watu wenye silaha kuendelea kutekeleza mauaji dhidi ya raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.