Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Wanaharakati kadhaa wakamatwa DRC

Wanaharakati wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanaomtaka rais Jospeh Kabila kuondoka madarakani kufikia tarehe 20 Desemba wamekamatwa na kuhojiwa na polisi.

Wanaharakati wa vuguvugu la Filimbi wakijiandaa kuandamana mjini Kinshasa, Oktoba 29.
Wanaharakati wa vuguvugu la Filimbi wakijiandaa kuandamana mjini Kinshasa, Oktoba 29. Sonia Rolley/RFI
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati sita wa vuguvugu la Filimbi wanashtakiwa kukiuka utaratibu, kusumbua umma na kuchochea uasi amesema Kanali Ezekiel Mwana Mputu Msemaji wa polisi akihojiwa na shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Katika harakati zao, zaidi ya waandamanaji thelathini wa "Filimbi" waliokuwa wakiimba nyimbo za kumtaka rais Kabila kuachia ngazi ifikapo desemba 20 wametawanyika na kunyanganywa mabango yao, huku polisi ikitumia mabomu ya machozi.

Nia na madhumuni ya maandamano yao ni kuuambia Umoja wa Afrika AU kwamba unawajibika vya kutosha katika mapinduzi ya kikatiba yaliyoamua Rais Kabila aendelee kubaki madarakani hadi 2018.

Wakati hayo yakijiri, jijini Lubumbashi (kusini-mashariki) mwa DRC, na mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, polisi wamekabiliana na mamia ya wanaharakati wa upinzani ambao walikuwa wametamatisha mkutano wa kisiasa ambapo jumla ya watu 29 wamekamatwa, 18 wa chama cha UDPS na 11 wa UNAFEC, mwishoni mwa wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.