Pata taarifa kuu
DRC-JOSEPH KABILA

Muungano wa Rassemblement nchini DRC wapinga makubaliano ya hivi karibuni

Chama kikuu cha upinzani nchini DRC chake Etiene Tshisekedi kimepinga makubaliano yaliyotiliwa sahihi siku ya jumanne ambayo yanaridhia raisi Joseph Kabila kusalia madarakani hadi mwaka 2018 kwa kuahirisha uchaguzi uliokuwa ufanyike mwaka huu.

Kiongozi wa chama cha Upinzani UDPS DRC Etienne Tshisekedi
Kiongozi wa chama cha Upinzani UDPS DRC Etienne Tshisekedi RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu wa chama UDPS Jean-Marc Kabund amesema Chama hiko kimekataa pendekezo hilo linalochelewesha uchaguzi na kukiukwa kwa katiba ya DRC.

Pendekezo hilo lilipitishwa na mamlaka na vyama kadhaa vya upinzani vilivyoshiriki mazungumzo ya kitaifa yaliyofanyika kuondoa hali ya mvutano iliyosababishwa na hofu kuwa huenda raisi Kabila atasalia madarakani hata mara muda wake utakapo tamatika mwezi Decemba.

Mnamo siku ya jumanne viongozi wa makundi hayo yaliyoshiriki mazungumzo walikusanyika na kusheherekea jijini Kinshasa kutiliwa sahihi kwa mkataba huo wenye kurasa 24.

Aidha Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault alisema uamuzi wa kuahirisha uchaguzi haukuwa suluhu ya mzozo unaolikabili taifa hilo bali ni raisi Kabila kutangaza kutowania tena kiti cha uraisi na kuandaa tarehe ya uchaguzi.

Mpango huo unafikiwa baada ya umoja wa Ulaya EU kutishia kuiwekea nchi hiyo vikwazo ikiwa uchaguzi hautafanyika 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.