Pata taarifa kuu
LIBYA-CHAD

Jenerali Khalifa Haftar apokelewa Ndjamena na Rais Déby

Libya inakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kiongozi wa serikali ya umoja ametoa wito kwa ajili ya mazungumzo kati ya pande zote ili kuepuka kuongezeka kwa machafuko. Wakati huo huo majeshi ya jenerali Haftar yamedhibiti mitambo ya kuzalisha mafuta, hali ambayo inatia wasiwasi jumuiya ya kimataifa.

Jenerali Khalifa Haftar karibu na mji wa Benghazi, Mei 17, 2014..
Jenerali Khalifa Haftar karibu na mji wa Benghazi, Mei 17, 2014.. REUTERS/Esam Omran Al-Fetori
Matangazo ya kibiashara

Jumanne wiki hii jenerali muasi alijielekeza katika mji mkuu wa Chad, Ndjamena. Alipokelewa na Rais Deby, ambaye alikuwa alimuomba kukutana naye.

Jenerali Khalifa Haftar akiongozana na ujumbe mkubwa alipokelewa na maafisa waandamizi wa Chad. Wakati huo alialikwa kwa chakula cha mchana kabla ya kupelekwa kwa viongozi wa juu.

Katika ajenda ya mazungumzo yao, hali ya usalama kusini mwa Libya, lakini hasa uwepo wa waasi wa Chad katika mpaka wa kaskazini mwa Chad. jambo ambalo lilipelekea Rais Idriss Deby kuamua kuwafuata mwenyewe, chanzo cha usalama kimeiambia RFI.

Kwa mujibu wa vyanzo vingine, majeshi ya jeneralil Haftar yalivamia siku za hivi karibuni visima vya mafuta, na hali hiyo ndio ilipelekea jenerali Haftar kujielekeza mjini Ndjamena. Jumuiya ya kimataifa ilikua na taarifa kwamba mkuu wa zamani wa majeshi yaliyopambana dhidi Gaddafi amekua haskii la mtu katika ngazi ya kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.