Pata taarifa kuu
MOROCCO-POLISARIO

Mkataba wa usitishwaji wa mapigano kukiukwa

Hati ya siri ya Umoja wa Mataifa imebaini kuwa mkataba wa usitishwaji wa mapigano uliyosainiwa mwaka 1991 na Morocco pamoja na kundi la waasi la Polisario Front ulikiukwa na pande zote mbili zinazopigania eneo la Sahara Magharibi.

MINURSO (ujumbe wa UN) ulitumwa miaka 25 iliyopita ili kusimamia mkataba wa usitishwaji wa mapigano katika eneo la Sahara Magharibi.
MINURSO (ujumbe wa UN) ulitumwa miaka 25 iliyopita ili kusimamia mkataba wa usitishwaji wa mapigano katika eneo la Sahara Magharibi. AFP
Matangazo ya kibiashara

Morocco na kundi la waasi la Polisario Front wamewatuma wanajeshi wao katika eneo lililo karibu na Mauritania.

Hati, iliyosainiwa tarehe 28 Agosti, imewasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hati hiyo inabainisha kuwa Morocco iliendesha kati ya tarehe 16 na 25 Agosti 2016, operesheni ambayo ilikuwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya kundi hilo la waasi katika mkoa wa Guerguerat, kusini mwa eneo la Sahara Magharibi, mbali ya ukuta wa kujihami uliyojengwa kama sehemu ya kila upande.

Ukuta huo wa kujihami ni kizuizi cha mchanga kiliyojengwa kwenye eneo la kilomita takriban 2.5 kati ya maeneo hayo mawili yanayoshikiliwa na pande hizo mbili hasimu.

Kwa mujibu wa waandishi wa waraka huo, operesheni ya Morocco "ilizinduliwa bila taarifa kwa MINURSO (Tume ya Umoja wa Mataifa kwa minajili ya kufanyika kura ya maoni katika eneo la Sahara Magharibi), kinyume na matakwa ya mkataba wa kijeshi No 1" uliyosainiwa kati ya pande mbili.

Operesheni ilizinduliwa "kwa msaada wa vikosi vinavyomilikiwa na polisi ya utawala wa kifalmer nchini Morocco".

Kuhusu kundi la waasi la Polisario Front, MINURSO inathibitisha kuwepo kwa askari 32 wenye silaha wa Polisario Front" katika eneo moja ndani ya eneo lililo karibu na Mauritania.

MINURSO inaona kwamba hali hiyo ni "ukiukaji" wa mkataba wa usitishwaji wa mapigano ambao inasimamia tangu mwaka 1991.

Umoja wa Mataifa umeitaka Rabat na Polisario "kujizuia" ili kuzuiakutokea kwa mapigano

Tangu mapema mwezi Agosti, Umoja wa Mataifa unaandaa "pendekezo rasmi" ili kuanzisha upya mazungumzo kuhusu Sahara Magharibi, ambayo kwa sasa yamesitishwa.

Mazungumzo kati ya Rabat na kundi la Laayoune yameshindikana kwa miezi kadhaa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.