Pata taarifa kuu
DRC - SIASA

Mazungumzo ya kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu nchini DRC, yang'oa nanga bila upinzani

Kamati ya Maandalizi kwa ajili ya mazungumzo ya kitaifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeanza kazi yake Jumanne ya Agosti 23, mjini Kinshasa chini ya uongozi wa mpatanishi Edem Kodjo.

Wafuasi wa upinzani wakiwa na picha ya kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini DRC, Etienne Tshisekedi, picha ya hivi karibuni.
Wafuasi wa upinzani wakiwa na picha ya kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini DRC, Etienne Tshisekedi, picha ya hivi karibuni. DR
Matangazo ya kibiashara

Chama cha UNC cha Vital Kamerhe, Muungano wa Rassemblement unaoongozwa na Etienne Tshisekedi, chama cha MLC cha Jean Pierre Bemba pamoja na chama kinachoongozwa na spika wa baraza la Senet Kengo wa Dondo havikushiriki katika uzinduzi huo vikihitaji kwanza masharti yao yatekelezwe.

Kwa mujibu wa Franck MWE DI Malila, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa chama cha Opposition Republicaine, chama hicho kinakataa kushiriki katika mazungumzo hadi mfumo wake uliopo ubadilishwe.

Akizindua Kamati hiyo mbele ya waangalizi wa Jumuiya ya kimataifa, Edem Kodjo, ameelezea masikitiko yake kufuatia kutokuwepo kwa wajumbe wa vyama hivyo vikubwa vya upinzani.

Kodjo amesema kuwa utaratibu huu wa mazungumzo utafanyika chini ya Katiba ya Congo na azimio 2277 la Machi 30, 2016 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, jambo ambali limeombwa na wapinzani.

Hayo yakijiri, shirika la raia limeonyesha kughadhabishwa na kitendo cha mpatanishi kuonyesha orodha ya wajumbe wake bila ya kushirikishwa na kusema wako amabo waliteuliwa wajumbe bila ya kutokea kwenye mashirika ya kiraia.

Kwa vyovyote hivyo, bado mzozo wa Congo utaendelea kuwa gumzo na kutatiza dhamiri ya wakongo na jumuiya ya kimataifa hadi pale ambapo suluhu ya kweli itapatikana hasa kwa kufaulu kuwashirikisha wadau wote nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.