Pata taarifa kuu
CONGO-UCHAGUZI-SIASA

Congo: Sassou-Nguesso aelekea kushinda uchaguzi

Nchini Congo-Brazzaville, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CNEI), iliopingwa na upinzani, imetangaza matokeo ya kwanza na ya muda ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais.

Denis Sassou Nguesso, Rais wa Congo Brazzaville akipiga kura mjini Brazzaville katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais, Jumapili Machi 20, 2016.
Denis Sassou Nguesso, Rais wa Congo Brazzaville akipiga kura mjini Brazzaville katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais, Jumapili Machi 20, 2016. © MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Matokeo hayo yanaonyesha kuwa Rais anayemaliza muda wake Denis Sassou-Nguesso anaongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi kwa 67.02% ya kura.

Kulingana na matokeo ya awali yaliyotolewa na tume ya uchaguzi (CNEI), Rais anayemaliza muda wake Denis Sassou-Nguesso huenda akashinda kwa 67.02% ya kura. Takwimu hii ni sambamba na matokeo ya maeneo 72 kati ya majimbo 111 na wilaya za nchi hiyo, kulingana na makadirio yetu, huku wapiga kura wakiwa kwenye kiwancgo cha 58%.

Katika nafasi ya pili ya raundi ya kwanza ya uchaguzi wa rais, Guy Brice Parfait Kolélas amepata 16.18%; jenerali Jean-Marie Michel Mokoko, anaongoza nafasi ya tatu kwa 7.5% ya kura. kiwango cha ushiriki katika hatua kilifikia kwenye 65.74%.

Matokeo haya ya awaliyanahusu majimbo na wilaya zote, ispokua mji wa Pointe-Noire, mji mkuu wa uchumi wa nchi hiyo, ambao ni ngome kuu ya upinzani. Katika mikutano ya kampeni za uchaguzi, wafuasi wa upinzani walikua wakifurika kwa wingi katika mji huo.

Uchaguzi "uliokunjwa"

Lakini katika makao makuu ya kampeni ya rais anaye maliza muda wake, ushindi, Jumanne hii usiku, haukua na mashaka. "Nadhani tunaweza tukatarajia ushindi mkubwa katika duru ya kwanza," Thierry Moungalla, mkurugenzi wa mawasiliano ya mgombea ameeleza, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika katika umati wa wafuasi wa chama madarakani na ambao utangazwa mapema Jumanne asubuhi.

Hata hivyo upinzani umeahidi kupambana ili kuonyesha kuwa uchaguzi huo uligubikwa na kasoro nyingi na kwamba matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi ni potofu na yenye upendeleo. Lakini baadhi ya wapinzani wamesema wako tayari kukabilia na utawala mitaani.

Uchaguzi huo umekuosolewa na Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Afrika, ukibaini kwamba uligubikwa na kasoro nyingi, hususan, kadi moja ya kupigia kura ilikua moja ya dalili za wizi wa kura, na kuharakia kutoa kalenda ya uchaguzi ilichangia uchaguz huo kuwa na mashaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.