Pata taarifa kuu
CONGO-SASSOU-KURA YA MAONI-SIASA

Kura ya “ndio” yashinda kura ya “hapana” Congo

Matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika Jumapili mwishoni mwa juma lililopita nchini Congo-Brazzaville yametangazwa na kuonyesha kura ya ndio imeshinda dhidi ya kura ya hapana.

Rais wa Congo Denis Sassou-Nguesso akipiga kura wakati wa kura ya maoni Oktoba 25, 2015.
Rais wa Congo Denis Sassou-Nguesso akipiga kura wakati wa kura ya maoni Oktoba 25, 2015. AFP PHOTO
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na matokreo hayo marekebisho ya katiba yanayomruhusu rais wa sasa kuwania kwa muhula wa tatu yameidhinishwa.

Kwa mujibu wa serikali ya Congo, asilimia 92 ya wapiga kura walioshiriki kura ya maamuzi kuhusu marekebisho hayo ya kikatiba Jumapili waliunga mkono marekebisho hayo.

Kuandaliwa kwa kura hiyo ya maamuzi kulikuwa kumezua maandamano wiki iliyopita na vyama vikuu vya upinzani viliisusia.

Hata hivyo upinzani umesema hautambui matokeo hayo na kudai kwamba kulikuwa na udanganyifu, huku ukibaini kwamba watu wengi hawakujitokeza kupiga kura.
Umoja wa Ulaya na Marekani zimekashifu kuandaliwa kwa kura hiyo, na kusema mazingra nchini Congo hayakuwa mwafaka kuwezesha kuandaliwa kwa kura ya maoni huru na ya haki.

Kulingana na Katiba iliyokuwepo , Rais Denis Sassou Nguesso alikuwa haruhusiwi kuwania kwa muhula mwingine kwa sababu amepitisha umri wa miaka 71 na pia amehudumu mihula miwili.

Rais Sassou Nguesso ni miongoni mwa viongozi wa sasa Afrika waliokaa madarakani muda mrefu zaidi. Aliingia mamlakani mara ya kwanza mwaka 1979.

Kwa sasa anamalizika muhula wa pili wa miaka saba. Alishinda uchaguzi mkuu 2009 kwa asilimia 79. Uchaguzi ambao ulisusiwa na nusu ya wagombea wa upinzani.

Serikali ya Ufaransa kutpia msemaji wa wizara ya mambo ya nje, Romain Nadal, imesema imetambua matokeo hayo.

Awali rais wa Ufaransa alimuonya Rais Denis Sassou Nguesso kutoitisha kura ya maoni, baada ya kukosolewa na upinzani wa Cingo na baadhi ya wanasiasa wa Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.