Pata taarifa kuu
CONGO-SASSOU-KURA YA MAONI-SIASA

Congo: Parfait Guy Brice Kolelas azingirwa nyumbani kwake na jeshi

Waziri wa zamani anayepinga kura ya maoni ya katiba, Guy Brice Parfait Kolelas anautuhumu utawala kutaka kumua kwa njaa.

Picha ya zamani ya Parfait Guy Brice Kolelas,  mwaka 2007.
Picha ya zamani ya Parfait Guy Brice Kolelas, mwaka 2007. AFP / Martin VAN DER BELEN
Matangazo ya kibiashara

Tangu Alhamisi, waziri huyo wa zamani anazingirwa nyumbani kwake akiwa pamoja na zaidi ya wafuasi wake thelathini. Parfait Kolelas amesema, askari wa walinzi wa rais wanamzuia mtu yeyote kuja kumtembelea.

Mmoja tu ambaye aliweza kuvuka vizuizi viliyowekwa na wanajeshi hao ni balozi wa Ufaransa ambaye alimletea chakula. Serikali inasema haina taarifa kuhusu hali hiyo.

Tangu Alhamisi wiki iliyopita, Guy Brice Parfait Kolelas na zaidi ya wafuasi wake thelathini wamezuiliwa nyumbani kwake. Hawawezi kuondoka katika nyumba hiyo au kupokea mtu yeyote. Askari hamsini wa walinzi wa rais wamezingira eneo anakoishi waziri huyo wa zamani.

Kolelas ambaye pia ana uraia wa Ufaransa, balozi wa Ufaransa alichangia kwa kulmetea chakula kilichokua kiliandaliwa na ndugu wa waziri huyo wa zamani.

Kwa siku kadhaa, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Afrika ya Kati, Abdoulaye Bathily, amekua akijaribu kusuluhisha ili mpinzani huyo awez kuwa huru kwa harakati zake. Upinzani pia umesema kwamba hautashiriki tena katika mazungumzo ya kisiasa kama hali hiyo itakua haijapatiwa ufumbuzi.

Upande wa serikali, wamejizuia kutoa maelezo yoyote. Chanzo cha serikali kimesema bila kuwa na aibu kuwahaina taarifa ya hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.