Pata taarifa kuu
CONGO-SASSOU-KUTAWAZWA

Congo: Denis Sassou Nguesso atawazwa kuwa mgombea urais

Rais wa Congo Denis Sassou Nguesso, Jumatatu hii, ametawazwa na chama chake tawala mjini Brazzaville kuwa mgombea katika uchaguzi wa urais wa Machi 20, chama cha PCT kimesema katika taarifa yake.

Denis Sassou Nguesso, Oktoba 22, 2010 jijini Montreux.
Denis Sassou Nguesso, Oktoba 22, 2010 jijini Montreux. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Katiba mpya ya Congo, ambayo ilianza kutekelezwa mwezi Novemba baada ya kupitishwa kwake wakati wa kura ya maoni iliyosusiwa na upinzani, inamruhusu Bw Sassou Nguesso, aliyezaliwa mwaka 1943 na ambaye yuko madarakani kwa zaidi ya miaka 30, kuwa mgombea kwa muhula wa tatu.

Kura ya maoni ilipigwa katika hali ya sintofahamu Oktoba 25, 2015.

Umoja wa Ulaya ulibaini kwamba " hali inayojiri nchini Congo-Brazzaville hairuhusu uchaguzi huru na wa uwazi" nchini humo. Hata hivyo kura hiyo ya maoni ilifanyika katika hali ya taharuki wakati ambapo upinzani uliwataka wafuasi wake kususia kura hiyo. ambayo haikua na shauku kubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.