Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-UFISADI

FIFA yaweka bayana mshahara wa Blatter mwaka 2015

Kwa mara ya kwanza Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetangaza Alhamisi hii kwamba Sepp Blatter alipokea Euro milioni 3.20 mwaka 2015, sawa na kiwango cha wastani cha zaidi ya Euro 270,000 kwa mwezi. Ni kwa mara ya kwanza FIFA kutangaza hadharani mshahara wa rais wa zamani wa shirikisho hilo.

Rais wa zamani wa FIFA Sepp Blatter akipongezwa kwa noti za Dola, Julai 20, 2015 katika Zurich
Rais wa zamani wa FIFA Sepp Blatter akipongezwa kwa noti za Dola, Julai 20, 2015 katika Zurich AFP
Matangazo ya kibiashara

Aidha, Shirikisho la kimataifa la Soka linabaini kwamba lilipoteza Dola milioni 122 (sawa na Euro milioni 107.7) katika mwaka 2015, nakisi yake ya kwanza tangu mwaka 2002, kwa sababu hasa ya gharama za kashfa ya rushwa zilioikumba, Shirikisho la Soka Duniani limearifu katika taarifa yake.

Kwa upande mwengine Katibu Mkuu wa zamani wa FIFA Jérôme Valcke, raia wa Ufaransa, ambaye tayari kusimamishwa kwa miaka 12 kwa kosa la mauzo ya tiketi za Fifa, na kwa sasa anakabiliwa na utaratibu wa kisheria, vyombo vya sheria vya Uswisi vimeliamblia shirika la habari la Ufaransa la AFP Alhamisi hii.

Ofisi ya Mwendesha mashitaka Mkuu wa Uswisi imeeleza katika taarifa iliyotuma kwa shirika la habari la Ufaransa la AFP kwamba limefungua kesi kwa kukabiliana na malalamiko mawili baada ya "tuhuma dhidi ya Jérôme Valcke katika uhusiano na uchunguzi ulioendeshwa na FIFA."

Vyombo vya sheria vya Uswisi vimeanza uchunguzi na vimesema kwamba vimefanya "mahojiano" bila hata hivyo watiuhumiwa kukamatwa.

Katibu Mkuu wa zamani wa FIFA, mwenye umri wa miaka 55, aliondolewa katika wadhifa wake Septemba 17 baadaya kufanyiwa uchunguzi kuhusu mauzo ya tiketi za michuano ya Kombe la Dunia 2014, kabla ya kufutwa kazi tarehe 13 Januari.

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) linakabiliwa na kashfa ya rushwa, baada ya viongozi wake kushutumiwa kupitisha mlango wa nyuma na kupewa hongo katika michuano mbalimbali ya kimataifa.

Jumatano wiki hii shirikisho hilo liliinyoshea kidole Afrika Kusini kutoa hongo kwa minajili ya kukubaliwa kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia 2010, licha ya Waziri wa Michezo wa Afrika Kusini kukana tuhuma hizo.

Viongozi kadhaa wa taasisi hii ya kimataifa waliachishwa kazi kutokana na madai ya rushwa. Hata hivyo Rais mpya wa shirikisho hilo, Gianni Infantino, ameapa kufanya kila aliwezalo ili FIFA ifidiwe na viongozi walioipaka matope, na ambao walipelekea taasisi hii kupoteza mamilioni ya fedha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.