Pata taarifa kuu
SOMALIA-SHAMBULIZI-USALAMA

Somalia: jeshi laimarisha ulinzi Mogadishu

Jeshi la serikali la nchini Somalia limeimarisha ulinzi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu, baada ya kufanyika kwa mauaji ya watu wasiopungua 30 katika shambulizi lililodaiawa kutekelezwa na Al Shabab, mjini Baidoa Kusini mwa nchi hiyo.

Askari wa Uganda wa AMISOM, katika jimbo la Bas-Shabelle Somalia, mwaka 2014.
Askari wa Uganda wa AMISOM, katika jimbo la Bas-Shabelle Somalia, mwaka 2014. AMISOM/TOBIN JONES
Matangazo ya kibiashara

Inaarifiwa kuwa milipuko miwili mikubwa ilitokea, katika mkahawa uliokuwa umejaa mashabiki wengi ambao walikuwa wakitazama mechi kati ya Manchester United na Arsenal, na kwamba miongoni mwa watu waliouawa ni pamoja na afisa wa serikali ya jiji hilo. Watu 61 wamejeruhiwa katika shambulizi hilo.

Maafisa wanasema walionusurika waliokolewa na wanajeshi wa Umoja wa Afrika (AMISOM) huku wakithibitisha watu wengine zaidi ya 20 waliuawa siku ya ijumaa katika mgahawa mwengine kufuatia shambulizi la Al Shabab.

Somalia imeendelea kukabiliwa na mashambulizi ya hapa na pale yanayotekelezwa na wanamgambo wa kiislam wa Al Shabab, licha ya kuwepo serikaliambayo ia majeshi yanayosaidiwa na wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika (AMISOM). Hata hivyo kikosi hiki kimefanya kazi kubwa, baada ya kurejesha kwenye himaya ya serikali dhaifu ya Somalia baadhi ya maeneo yaliokuwa yakishikiliwa na wanamgambo wa Al Shabab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.