Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-AU

Somalia: wanajeshi wa serikali waukomboa mji wa Merca

Vikosi vya serikali ya Somalia vikishirikiana na wanajeshi wa Umoja wa Afrika (AMISOM) wameukomboa mji wa Merca kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Alshabab ambao waliuteka mji huo siku ya ijumaa, kwa mujibu wa serikali. 

Wanajeshi wa Kenya wakiwa kwenye moja ya kambi yao kukabiliana na wapiganaji wa Al-Shabab
Wanajeshi wa Kenya wakiwa kwenye moja ya kambi yao kukabiliana na wapiganaji wa Al-Shabab Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab waliuteka mji wa Merca, nchini Somalia, Ijumaa wiki hii bila hata hivyo kumwagika damu baada ya askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika (AMISOM) kuondoka katika mji huo.

Umoja wa Afrika siku ya ijumaa ulikataa katu katu madai ya mji huo kutekwa na Al-shabab, ukibaini kwamba wanajeshi wake waliondoka kwa mkakati.

Mwanajeshi mmoja wa Somalia ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kwamba vikosi vya Somalia vikishirikiana na vile vya Umoja wa Afrika vimechukua udhibiti wa mji wa Merca na hali imerejea kuwa tulivu.

Ijumaa wiki hii Mkuu wa jimbo la Shebelle nchini Somalia alithibitisha taarifa ya kutekwa kwa mji huo, akibaini kwamba wapiganaji wa Al-Shabaab waliuteka mji wa Merca baada ya kuondoka kwa vikosi vya Umoja wa Afrika.

Askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika (AMISOM) waliondoka tu katika mji huo na wapiganaji wa Al-Shabab wakaingia.

“Mji wa Merca umetekwa bila ya damu kumwagika, alisema Ibrahim Said”, akiliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kimetangaza.

Vikosi vya Umoja wa Afrika viliwahi kuudhibiti mji huo wa Bandari kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.