Pata taarifa kuu

UN: “ juhudi zapaswa kufanyika kwa kutokomeza Al Shabab ”

Umoja wa Mataifa unasema kuwa, zaidi ya wakimbizi elfu 7 raia wa Somalia waliokuwa wanaishi nchii Yemen wamerudi nyumbani kwa sababu ya mapigano yanayoendelea.

Mpiganaji wa Al shabab, kundi lenye mafungamano na Al Qaeda.
Mpiganaji wa Al shabab, kundi lenye mafungamano na Al Qaeda. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Nicholas Kay mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, amesema kuwa wakati raia hao wakirudi nyumbani, juhudi zinanstahili kufanyika kuhakikisha kuwa wanagambo wa Al Shabab hawapati uungwaji mkono kutoka kwa waasi nchini Yemen.

Raia hao wa Somalia wanarudi nyumbani kuungana na wenzao zaidi ya Milioni tatu wanaokabiliwa na baa la njaa na kukabiliana na vitisho vya Al Shabab.

Wakti huo huo mwakalishi wa Umoja wa mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay amesema anatiwa na hofu kuwa huenda mashambulizi ya wanamgambo wa Al shabab yakaongezeka ikiwa hatua ya kuondoa majeshi ya Burundi itafanyika nchini Somalia.

Hivi karibuni Marekani ilitangaza kupunguza kiasi cha pesa inachotoa kwa majeshi ya Burundi baada ya shutuma kuwa jeshi hilo limejihusisha katika vitendo vya ukiukwaji wa haki za binaadam lilipokua likijaribu kuzima jaribio la mapinduzi lililoendeshwa na jenerali Godefroid Niyombare.

Kay amesema majeshi ya Umoja wa Afrika yanahitaji msaada kuweza kupambana na Al Shabaab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.