Pata taarifa kuu
CAR-UCHAGUZI-SIASA

CAR: raia wapiga kura kwa ajili ya amani

Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamepiga kura Jumapili hii katika utulivu kwa kuchagua kati ya Mawaziri Wakuu wawili wa zamani Anicet Georges Dologuélé na Faustin Archange Touadéra, rais ambaye ataiondoa nchi hiyo katika ghasia za kijamii zinazodumu kwa sasa miaka mitatu.

Mtu huyu akibeba vifaa vya uchaguzi katika mji wa Bangui kwa uchaguzi wa urais na wa wabunge nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Februari 14, 2016.
Mtu huyu akibeba vifaa vya uchaguzi katika mji wa Bangui kwa uchaguzi wa urais na wa wabunge nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Februari 14, 2016. © REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya wapiga kura milioni mbili wametakiwa kumchagua mmoja kati ya wagombea wawili wa urais, wote wenye umri wa miaka 58.

Zoezi la kupiga kura limeanza saa 12:00 asubuhi (sawa na saa 11:00 asubuhi saa za kimataifa) katika baadhi ya vituo vya kupigia kura, na vituo vingine vilichelewa kufungua. Vituo vya kupigia kura vimetakiwa rasmi kufungwa saa 10:00 alaasiri (sawa na saa 9:00 alaasiri saa za kimataifa).

Matokeo ya kwanza yatajulikana hivi karibuni.

"Tumetakiwa kupiga kura leo", Paterne, mwenye umri wa miaka zaidi ya arobani, mkazi wa Bangui, ameliambia shirika la habari la ufaransa, wakati alipokua akisubiri kupiga kura katika shule ya Benz-6 mjini Bangui. "Huu ni uchaguzi wa kuchukua hatua. Kwa mara ya kwanza, tunafanya uchaguzi halisi ili kuvipa mgongo vita", Paterne amesema.

Lakini katika mji wa Bangui, vituo vya kupigia kura havikushuhudia ushiriki kama ule wa duru ya kwanza ya uchaguzi wa Desemba 30, wakati foleni ndefu zilishuhudiwa. Katika vituo vingi, kiwango cha ushiriki kimezidi 50%, chini ya masaa mawili kabla ya kumalizika kwa zoezi la kupiga kura.

Katika mikoa pia, ambapo zoezi hili limeendelea katika hali ya utulivu, wapiga kura hawakua wengi katika miji ya Obo (kaskazini masharuki), Bambari (mashariki) au Berberati (kusini).

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Taifa ya Uchaguzi (ANE), Marie Madeleine N'Kouet Hoornaert, "kwa ujumla uchaguzi umekwenda vizuri, isipokuwa baadhi ya matatizo ambayo yamejitokeza katika baadhi ya vituo vya kupigia kura vya" baadhi ya mkoa na katika mji wa Bangui ambapo wapiga kura wamefukuzwa.

Katika nchi hii ya watu milioni 4.8, wapiga kura, ikiwa ni pamoja na Wakristo na Waislamu, walijiandikisha kwa wingi kwenye orodha ya uchaguzi.

Bw Dologuélé, aliyewekeza katika biashara, amepewa nafasi kubwa ya kushinda baada ya kuongoza katika duru ya kwanza kwa (23.78%), hasa baada ya kuungwa mkono na chama cha KNK chama Bozize.

Zoezi la uhesabuji a kura linaendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Wachunguzi wakihesabu kura katika kitongoji cha PK5 mjini Bangui, Jumapili hii, Februari 14, 2016.
Wachunguzi wakihesabu kura katika kitongoji cha PK5 mjini Bangui, Jumapili hii, Februari 14, 2016. REUTERS/Siegfried Modola

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.