Pata taarifa kuu
KENYA-ICC-SIASA-SHERIA

Raila Odinga amshtumu Rais Kenyatta

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amemtuhumu Rais Uhuru Kenyatta kwa kuwakodi mashahidi ili kumfikisha naibu rais William Ruto katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC anakoshtakiwa kwa kufadhili machafuo ya baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007.

Raila Odinga, kiongozi wa upinzani nchini Kenya.
Raila Odinga, kiongozi wa upinzani nchini Kenya. REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Odinga amesema Rais Kenyatta amemtumia mfanyikazi wake ambaye kwa sasa ni mbunge wa serikali Moses Kuria kuwahonga mashahidi dhidi ya Ruto.

Haya yanajiri baada ya Moses Kuria kujitokeza na kukiri kuwa ni kweli aliwatafuta mashahidi kwenda kusema uongo dhidi ya Ruto.

Odinga ameongeza kuwa naibu wa rais wa sasa William Ruto alikuwa mshirika wake katika chama cha ODM na hivyo chama chake hakingemfikisha Hague kama inavyodaiwa na wapinzani wao.

Matamshi haya ya Odinga yamekanushwa vikali na Bwana Kuria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.