Pata taarifa kuu
KENYA-UPINZANI-Siasa-Haki za binadamu

Kenya: mvutano unaendelea kuhusu hatua ya serikali yakupokonya aridhi

Wabunge nchini Kenya wametofautiana vikali kuhusu iwapo rais wa taifa hilo Uhuru Kenyatta alikuwa na mamlaka ya kufutilia mbali hati miliki ya ardhi zipatazo laki tano, huku wito ukitolewa na baadhi ya viongozi kwa tume ya kitaifa ya ardhi ifutwe.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta atangaza hatua ya serikali yake ya kuchukua ardhi ya ekari laki 5 kwenye mji wa Lamu zinazomilikiwa kinyume cha sheria.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta atangaza hatua ya serikali yake ya kuchukua ardhi ya ekari laki 5 kwenye mji wa Lamu zinazomilikiwa kinyume cha sheria. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Katika hatua nyingine waziri wa kazi nchini humo, Kazungu Kambi ametishia kumfungulia mashtaka aliyekuwa waziri wa ardhi wakati huo, James Orengo ambaye jana alimtaja Kambi kuwa miongoni mwa viongozi waliochukua aridhi kwa nguvu kwenye eneo la Lamu.

Kauli hii ya Orengo ndiyo iliyomsukuma Kazungu Kambi kujibu mapigo kwa kukanusha madai ya kuwa na yeye amehusika katika kunyang'anya ardhi kwa nguvu kwenye eneo la Lamu na kusisitiza kuwa ardhi anayoimiliki anaimiliki kihalali.

Waziri huyu wa kazi anasema kuwa hana shaka dhidi ya tuhuma alizopewa na Orengo na kuhoji uhalali wake wakati akiwa waziri wa ardhi kunyang'anya watu ardhi na kwamba hata yeye anahusika.

Mvutano huu wa maneno na tuhuma dhidi ya viongozi walioko madarakani na wale wa upinzani unakuja ikiwa zimepita siku chache tu toka rais Uhuru Kenyatta atangaze serikali yake kuchukua ardhi ya ekari laki 5 kwenye mji wa Lamu zinazomilikiwa kinyume cha sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.