Pata taarifa kuu
KENYA-Usalama

Kenya : Shambulio la gruneti lasababisha hasara katika mji wa Wajir

Mtu moja ameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika shambulio la gruneti liliyorushwa na mtu mwenye silaha dhidi ya mgahawa ulioko katika mji wa Wajir, kaskazini mashariki mwa Kenya, polisi imethibitisha.

Shambulio la gruneti lasababisha kifo cha mtu mmoja na wengine wengi kujeruhiwa katika mji wa Wajir, nchini Kenya
Shambulio la gruneti lasababisha kifo cha mtu mmoja na wengine wengi kujeruhiwa katika mji wa Wajir, nchini Kenya REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

“Wahanga wamepelekwa hospitalini wilayani Wajir. (...) Mmoja kati ya majeruhi amefariki kwa majeraha ya risase”, amesema mkuu wa polisi katika wilaya ya Wajir, David Kuria.

Shambulio hilio limetokea jumatatu hii jioni katika eneo linalokabiliwa ba mdororo wa usalama liliyoko kwenye mpaka na Somalia, ambayo inakabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Hakunda kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo. Hata hivo wanamgambo wa kisomalia wa kundi la Al Shabab lenye mafungamano na kundi la Al Qaeda, waliendesha hivi karibuni mashambulizi katika eneo hilo.

Eneo hilo linakabiliwa na mapigano ya mara kwa mara kati ya kabila kutoka jamii ya kisomalia, ambayo yamesababisha vifo vya watu 80 tangu mwezi Mei, kutokana na mzozo kuhusu aridhi na mifugo.

Eneo hilo linakabiliwa pia na mdororo wa kiusalama kutokana na makundi ya watu wenye kubebelea silaha.

Tangu katikati mwa mwezi wa Juni, Kenya inakabiliwa na mashambulizi na mauaji ya kikatili, ambayo kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu, limesababisha vifo vya watu87 katika eneo pekee la ufukwe wa bahari Hindi.

Kundi la Al Shabab lilikiri kuhusika na mashambulizi hao, likibaini kwamba ni ulipizaji kisase dhidi ya wanajeshi wa Kenya waliotumwa nchini Somalia kujiunga na kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika (Amisom), kwa kukabiliana na wanamgambo wa kiislamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.