Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-UCHAGUZI-SIASA

Côte d'Ivoire: wagombea watangazwa, Ouattara apewa nafasi kubwa ya ushindi

Orodha ya mwisho ya wagombea wa uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Oktoba 25 nchini Côte d'Ivoire, iliyotangazwa Jumatano wiki hii na Baraza la Katiba, haikuwashangaza wengi: rais anayemaliza muda wake Alassane Ouattara atawania muhula wa pili dhidi ya upinzani uliogawanyika.

Rais wa Baraza la Katiba akitangaza orodha ya mwisho ya wagombea wa uchaguzi wa urais Oktoba 25.
Rais wa Baraza la Katiba akitangaza orodha ya mwisho ya wagombea wa uchaguzi wa urais Oktoba 25. AFP PHOTO / SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Jumla ya wagombea kumi watakuwa katika duru ya kwanza.

Alassane Ouattara, ambaye anaweza kujivunia rekodi nzuri ya kiuchumi, amepewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo muhimu kwa ajili ya kuleta utulivu nchini humo baada ya machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2011.

Zaidi ya raia 3,000 wa Côte d'Ivoire waliuawa katika kipindi cha miezi mitano ya machafuko yaliyosababishwa na kukataa kwa Laurent Gbagbo kutambua ushindi wa Alassane Ouattara, baada ya muongo mmoja wa mgogoro wa kisiasa na kijeshi nchini Côte d'Ivoire

Waangalizi wengi wanaona kuwa Bw Ouattara, mwenye umri wa miaka 73, atapata ushindi katika duru ya kwanza, matumaini ambayo kambi ya rais imeweka uwazi.

Si chini ya watu 33 waliwasilisha fomu zao za ugombea, na kutangazwa kwa orodha na Baraza la Katiba inaonekana ni kipenga cha kuanza kwa kampeni, hata kama kampeni hizo zinatakiwa kuanza Oktoba 9.

Baraza la Katiba,linaloongozwa na Mamadou Koné anayechukuliwa kama mtu wa karibu wa Alassane Ouattara, hatimaye aliwafuta watu 23 kwenye orodha ya wagombea 33 waliowasilisha fomu zao za kugombea kwa Baraza hilo ( fomu 22 hazikupokelewa na moja haienezi masharti).

Wapinzani wakuu wa Bw Ouattara ni Waziri Mkuu wa zamani (katika miaka ya 2005-2007) Charles Konan Banny, Pascal Affi N'Guessan, mgombea wa chama cha FPI cha Rais wa zamani Laurent Gbagbo au Spika wa zamani wa Bunge Mamadou Koulibaly. Watataka kumsukuma Alassane Ouattara katika duru ya pili na kisha kujaribu kujiunga pamoja ili wamuangushe katika duru ya pili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.