Pata taarifa kuu
LIBYA-IS-MAPIGANO-USALAMA

Libya: askari watano wauawa katika ghasia Benghazi

Askari watano wa jeshi la serikali inayotambuliwa kimataifa ya Libya wameuawa katika mapigano na wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS) na kumetokea mlipuko wa bomu la kutegwa ardhini katika mji wa Benghazi (mashariki), shirika la habari lililo karibu na serikali La LANA limearifu Jumatatu wiki hii.

Askari wa Libya katika mji wa Benghazi, Februari 28, 2015.
Askari wa Libya katika mji wa Benghazi, Februari 28, 2015. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Likimnukuu msemaji wa jeshi, Miloud Zouai, shirika la habari la LANA limetoa leo Jumatatu taarifa ya kifo cha kamanda wa vikosi Maalum, Imad el-Jazoui, na askari wake watatu waliojeruhiwa " kufuatia mlipuko wa bomu la kutegwa ardhini katika eneo la Laythi " katikati mwa Benghazi.

"Jazoui ameuawa (Jumatatu) wakati alikua akiendesha msako katika nyumba moja katika eneo Laythi ", chanzo hicho kimeeleza.

Awali LANA ilitangaza Jumapili Agosti 30 kifo cha askari wanne na wengine 22 kujeruhiwa katika safu ya " jeshi na vikosi ambavyo vinashirikiana wakati wa mapigano makali katika eneo la Hawari na tawi kundi la Islamic State IS nchini Libya ".

" Mapigano makali na silaha za kila aina yanaendelea kati ya jeshi na makundi ya kigaidi katika eneo la Hawari ", limebaini shirika la habari la LANA, likikinukuu chanzo cha kijeshi ambacho kimeeleza kuwa jeshi la serikali inayotambuliwa kimataifa ya Libya linaendelea kusonga mbele katika sekta ya kusini ya Benghazi (kwenye umbali wa maelfu ya kilomita mashariki mwa mji wa Tripoli).

Miongoni mwa makundi yenye silaha kuna wapiganaji wa kiislam wenye itikadi kali wa Ansar al-Shariah, kundi lenye mafungamano na Al Qaeda, na Islamic State, ambalo lilianzisha harakati zake nchini Libya mwaka jana na tayari lilikiri kuhusika na mashambulizi mbalimbali katika mji huu.

Libya imeendelea kukumbwa na machafuko tangu kuanguka kwa utawala wa Gaddafi, kati ya wanamgambo, huku kukiendelea kushuhudiwa nchini humo mabaraza mawili ya bunge na serikali mbili, kila upande ukidai kuwa ndio halali. Serikali moja imetenga makao yake makuu mjini Tripoli na nyingine mjini Tobruk (mashariki), na hii ndio inatambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.