Pata taarifa kuu
MAREKANI-LIBYA-MASHAMBULIZI-USALAMA

Mokhtar Belmokhtar asadikiwa kuuawa

Jeshi la Marekani limeendesha mashambulizi ya angani usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili mwishoni mwa juma hili lililopita nchini Libya, mashambulizi ambayo yamekua yakimlenga Mokhtar Belmokhtar, Pentagon imethibitisha.

Mashambulizi ya Marekani yameendeshwa na ndege aina ya F-15.
Mashambulizi ya Marekani yameendeshwa na ndege aina ya F-15. Reuters/US Air Force/Senior Airman Matthew Bruch/Handout
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa yenye makao yake Tobruk imebaini kwamba mwanajihadi huyo kutoka Algeria ameuawa katika operesheni hiyo ya kijeshi, taarifa ambayo haijathibitishwa na Marekani.

Watu wengi wamekua wakijiuliza iwapo Mokhtar Belmokhtar ameuawa. Taarifa hiyo imethibitishwa jana Jumapili jioni na serikali ya Libya yenye makao yake Tobruk. Mokhtar Belmokhtar, raia wa Algeria ambaye amekua akisakwa, huenda ameuawa wakati wa mashambulizi ya angani ya Marekani usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, katika jimbo la Ajdabiya, mashariki mwa Libya. Mokhtar Belmokhtar ni kiongozi wa kundi linalodaiwa kuwa la kigaidi la Al-Mourabitoune.

Mashambulizi ya Marekani yamekua yakimlenga Mokhtar Belmokhtar, lakini Pentagon inaendelea kusubiri uchunguzi uliyo sahihi kabla ya kuthibitisha matokeo ya operesheni.

" Belmokhtar alionekana akijihusisha na ugaidi tangu miaka kadhaa iliyopita. Ni mtu ambaye alijiunga na kujitoa muhanga kupigania kundi la Al-Qaeda," amesema Kanali Warren, msemaji wa Wizara ya ulinzi ya Marekani.

Mokhtar Belmokhtar amekua akitangazwa mara kadhaa kuwa ameuawa, hususan mwezi April uliyopita na vyombo vya habari vya Algeria, au pia mwaka 2013, wakati jeshi la Chad lilipothibitisha kuwa lilimuua wakati wa operesheni zake nchini Mali.

Iwapo kifo chake kitathibitishwa, mashambulizi yatakuwa mafanikio ya kweli katika vita dhidi ya ugaidi ambavyo vinaendeshwa na Marekani. Operesheni ya mwisho ya Marekani nchini Libya ilifanyika mwaka mmoja uliyopita, wakati ambapo kikosi cha Marekani kilipowasili katika ardhi ya Libya ili kumkamata Abou Khattala, aliyetuhumiwa kushiriki katika shambulio la Benghazi, shambulizi ambalo liligharimu maisha ya balozi Christopher Stevens mwaka 2012.

Pentagon inatoa maelezo machache, lakini inajulikana hata hivyo kwamba ndege F-15 ziliendesha mashambulizi usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili mwishoni mwa juma hili.

Mokhtar Belmokhtar anahusishwa katika shambulio lililotokea mwezi wa Januari mwaka 2013 dhidi ya kituo cha gesi cha In Amenas nchini Algeria, shambulio ambalo liligharimu maisha ya watu 38, ikiwa ni pamoja na raia wa tatu wa Marekani. Tangu wakati huo Mokhtar Belmokhtar alianza kusakwa na Idara ya ujasusi ya Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.