Pata taarifa kuu
NIGERIA-JAMII-USALAMA

Kizaaza Nigeria: watoto wauzwa au kutumiwa kwa imani za kishirikina

Polisi wa Nigeria wamevamia zahanati moja iliyoko katika mji wa Aba kusini mashariki mwa nchi hiyo ambako wameokoa wasichana 32 wanaodaiwa kuwa walikuwa wakishikiliwa na genge la wauza binadamu.

Nigeria inakabiliwa na biashara ya binadamu, hasa watoto. watoto wamekua wakiuzwa na kutumiwa kwa kutumiwa katika maslahi mbalimbali.
Nigeria inakabiliwa na biashara ya binadamu, hasa watoto. watoto wamekua wakiuzwa na kutumiwa kwa kutumiwa katika maslahi mbalimbali. Reuters/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Wasichana hao walio kati ya umri wa miaka 15 na 17, walizuiliwa ndani ya vyumba na kutumiwa kwa ajili ya kupata watoto, amesema mkuu wa polisi wa jimbo la Abia. Madhumuni ya watoto wanaozalishwa ni kuuzwa kwa waganga wanaowahitaji kwa shughuli za ushirikina na wengine labda kuwapatia watu wanaohitaji kizazi.

Lakini mmiliki wa hospitali hiyo amekanusha madai kwamba anaendesha biashara ya kuzalisha watoto wa kuuzwa, na kuongezea kusema kuwa ni hospitali ya kuwasaidia wasichana wanaoshika mimba kabla ya wakati wao. Shirika linaloshughulikia maslahi ya watoto,Unicef linakadiria kuwa hadi watoto 10 huuzwa kila siku kote nchini Nigeria ambako biashara ya binadamu inashika nafasi ya tatu katika visa vya uhalifu baada ya rushwa katika uchumi wa nchi na biashara ya mihadarati.

Hata hivyo, mwandishi wa shirika la habari la Ufaransa AFP, Mbah, mwenye makao yake katika mji wa pwani kusini mwa Nigeria wa Port Harcourt amesema kuwa wahalifu wanapokamatwa si kawaida kuchukuliwa hatua au kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Kamishna wa Polisi wa Jimbo la Abia Bala Hassan amesema kuwa watoto wanne, ambao tayari walikuwa wameisha uzwa wakisubiri waliowanunua kuwachukuwa nao walinusuriwa katika operesheni hiyo.

Upelelezi wa shirika la kujitolea kupambana na biashara haramu ya binadamu nchini Nigeria limesema kuwa upelelezi wake umezua kua watoto wachanga wanafikia kiwango cha hadi dola za Marekani 6,400 kila mmoja ikitegemea pia jinsia ya mtoto.

Mtoto wa kiume ana bei kubwa zaidi, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC.
Katika sehemu za nchi ambako watoto hufanywa kafara inaaminika mwili wa mtoto mchanga hufanya mazingaombwe kuwa makali sana.

Wengine huuzwa kwa watu wanaohitaji watoto. Wanawake ambao hawajaolewa nchini Nigeria, wenye uwezo mdogo wanakabiliwa na matatizo wanaposhika mimba. Mara nyingi hutengwa na jamii zao.

Mwandishi Wetu mjini Abuja anasema kuwa wasichana ambao hujikuta katika hali ya uja uzito mara nyingi hulazimika kwenda katika hospitali ambazo zitaficha siri yao na matokeo yake ni kuwaacha watoto kwa wafanya biashara. Baadhi ya wasichana walionusurika huko Abia waliambia polisi kuwa baada ya watoto wao kuuzwa walipewa doka 170 na mmiliki wahospitali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.