Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-MASHAMBULIZI-USALAMA

Boko Haram yazidisha mashambulizi Maiduguri

Watu 20 wameuawa katika kituo cha mabasi mjini Maiduguri nchini Nigeria baada ya mwanamke mmoja aliyekuwa amejifunga mabomu kujilipua.

Soka la samaki ambapo kulitokea mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga, Juni 22 mwaka 2015, Maiduguri.
Soka la samaki ambapo kulitokea mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga, Juni 22 mwaka 2015, Maiduguri. AFP PHOTO/STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Walionusurika katika shambulizi hilo wamesema mwanamke huyo kabla ya kujipulia alionekana kama muuza samaki na baadaye akajilipua.

Mji wa Maiduguri umeendelea kushuhudia mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa kundi la Boko Haram ambalo limeendelea kudhofisha hali ya usalama Kaskazini mwa nchi hiyo na katika nchi jirani.

Hivi karibuni Muhammadu Buhari, rais mpya wa Nigeria, alionyesha nia yake ya kuchukua hatamu ya uongozi wa jeshi dhidi ya wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram. Buhari aliomba marais wenzake wa nchi tano kutoka Ukanda wa Afrika Magharibi kuchukua uongozi wa jeshi la Ukanda huo wakati wote wa “juhudi za vita”.

Mbali na nia hii, mkutano wa Abuja, ambao uliwaleta pamoja marais wa nchi nyingine za muungano ikiwa ni pamoja na Cameroon, Chad, Niger na Benin, ulitoa idadi ya mapendekezo.

Katika mkutano huo kulianzishwa katika hali ya ufanisi uongozi wa jeshi la pamoja kutoka nchi hizo tano. Yakiwa yalizinduliwa rasmi Mei 25, makao makuu ya kikosi hicho ni ya muda mpaka sasa. Karibu dola milioni 30 zinahitajika ili kikosi hiki kihamiye katika majengo mapya, ambayo yatakua kama makao yake makuu.

Nchi hizi tano pia zilikubaliana kuwatuma wanajeshi wao kabla ya tarehe 30 Julai mwaka 2015. Kikosi hiki, kama ilivyopangwa, kitakua chini ya uongozi wa afisa wa jeshi kutoka Nigeria, meja jenerali Buratai. Naibu mkuu wa kikosi atakua raia wa Cameroon, na kila mwaka uongozi utakua ikibadilishwa. Mkuu wa majeshi atakua afisa wa ngazi ya juu kutoka Chad, na kila mwaka kutakua mabadiliko kwenye nafasi hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.