Pata taarifa kuu
BURUNDI-USALAMA-SIASA

Hali ya sintofahamu yaripotiwa kaskazini mwa Bujumbura

Milio ya risasi na zana nzito nzito za kijeshi vimeendelea kusikika katika wilaya za Cibitoke na Kinama, Kaskazini mwa mji wa Bujumbura nchini Burundi. Mpaka saa tisa Alaasiri Jumatano wiki hii hakuna mtu yeyote aliye kuwa akiingia au kutoka katika wilaya ya Cibitoke.

Polisi ikiwatawanya waandamanaji katika wilaya ya Buterere, kaskazini magharibi mwa jiji la Bujumbura, Mei 12 mwaka 2015.
Polisi ikiwatawanya waandamanaji katika wilaya ya Buterere, kaskazini magharibi mwa jiji la Bujumbura, Mei 12 mwaka 2015. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Wilaya ya Cibitoke na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Kinama yamezingirwa na wanajeshi, huku kukiendelea kusikika miliyo ya risasi na maguruneti. Watu saba kutoka a,bao sita ni kutoka familia moja wameuawa na nyumba yao kuchomwa moto.

Mashahidi wamesema kuwa askari polisi zaidi ya kumi wameuawa, lakini msemaji wa polisi Pierre Nkurikiye amenaini kwamba askari polisi mmoja ameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa.

Wakati huo huo usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii miliyo ya risasi imesikika katika wilaya mbalimbali za mji wa Bujumbura kwa muda wa zaidi ya masaa manne.

Wanajeshi na askari polisi wengi walionekana kwenye barabara inayotoka inayotoka mjini kati Bujumbura kuelekea wilayani Kinama, Kaskazini mwa Bujumbura.

Hayo yanajiri wakati wananchi wa Burundi leo Jumatano wamedhimisha kumbukumbu ya miaka 53 toka taifa hilo lilipojipatia uhuru wake toka kwa wakoloni wa Ubelgiji July 1, 1962, wakati huu taifa hilo likishuhudia mzozo wa kisiasa.

Sherehe zimefanyika jijini Bujumbura na katika maeneo mengine ya nchi.

Akizungumzia siku hii, rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amewataka wananchi wake kuwa watulivu wakati huu nchi yake ikipitia kipindi kigumu cha kisiasa, huku akipongeza namna ambavyo wananchi walishiriki zoezi la uchaguzi wa wabunge na ule wa Serikali za mitaa kwa amani.

Kwenye hotuba yake iliyorushwa kupitia njia ya televisheni na redio, rais Nkurunziza ameitaka jumuiya ya kimataifa ambayo ilisusia kushiriki kwenye uchaguzi huo, kuacha kuingilia uhuru wa nchi yake na kwamba katiba imezingatiwa katika kufanya uchaguzi huu.

Kauli ya Nkurunziza anaitoa wakati huu ambapo Umoja wa Afrika wala Umoja wa Mataifa, haukutuma waangalizi wake kwenda nchini Burundi, kwa kile jumuiya hizo ilichodai kuwa hakukuwa na mazingira mazuri ya kufanyika uchaguzi ulio huru na haki.

Rais Nkurunziza ametumia hotuba yake kuiomba jumuiya ya kimataifa badala ya kuingilia masuala yake ya ndani, ishirikiane na Serikali yake katika kuwaletea wananchi maendeleo pamoja na kudumisha amani ya nchi.

Maadhimisho ya mwaka huu ya Uhuru yanafanyika wakati ambapo nchi ya Burundi inashuhudia mzozo mkubwa wa kisiasa ambapo wanasiasa wa upinzani wamesusia kushiriki uchaguzi wa nchi hiyo huku wakishinikiza pia rais Nkurunziza asiwanie urais kwa muhula wa watatu.

Machafuko ya nchi ya Burundi yamechangiwa pakubwa na uamuzi wa rais Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania urais kwa muhula wa tatu, jambo ambalo upinzani unadai kuwa ni kinyume na katiba ya nchi na azimio la Arusha ambalo linatoa nafasi ya vipindi viwili tu vya urais.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa maadhimisho ya mwaka huu hayana msingi wowote kwa wananchi kwakuwa nchi yao inakabiliwa na hali mbaya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.