Pata taarifa kuu
BURUNDI-UCHAGUZI

chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD chaongoza katika baadhi ya maeneo

Kura zimeendelea kuhesabiwa nchini Burundi baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge na madiwani hapo jana, uchaguzi ambao ulifanyika katika hali ya hofu ya kutokea kwa mashambulizi. Upinzani ambao unapinga muhula wa 3 wa rais Pierre Nkurunziza unasema uchaguzi huo ni maigizo. katika maeneo kadhaa chama tawala chaonekana kuongoza katika baadhi ya maeneo.

mwanamama akipiga kura katika Mkoa wa Ngozi, wakati wa uchaguzi uliofanyika jana juni 29. 2015.
mwanamama akipiga kura katika Mkoa wa Ngozi, wakati wa uchaguzi uliofanyika jana juni 29. 2015. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Hali ya Usalama imeendelea kushuhudiwa wakati huu kura zikiendelea kuhesabiwa, licha ya kusikika kwa milio ya risase katika usiku wa kuamkia leo katika baadhi ya mitaa ya manispaa ya jiji la Bujumbura.

Matokeo ya uchaguzi yanataraji kutolewa katika siku mbili zijazo, baada ya kukusanya kura zote, ambapo matokeo ya awali katika baadhi ya maeneo yameanza kutolewa yakionyesha kuongozwa na chama tawala cha CNDD-FDD.

Pacifique Nininahazwe mmoja kati ya viongozi wa mashirika ya kiraia wanaopinga muhula wa 3 wa rais Pierre Nkurunziza amesema kwamba wala hapakuwa na uchaguzi.

Hapo jana jioni baada ya zoezi la upigaji kura ambapo vituo vilipoanza kufunga, tume ya uchaguzi ilikuw ahaina uwezo wa kutowa takwimu za watu walioshiriki hadi siku mbili au tatu zijazo.

Hata hivyo ushindi wa chama tawala cha CND-FDD hautokubalika na upinzani na hata Jumuiya ya Kimataifa ambayo ililaani maandalizi duni ya uchaguzi huo na kupendekeza kuahirishwa, jambo ambalo lilitupiliwa mbali na serikali.

Charles Nditije mmoja kati ya viongozi wa upinani amesema huu haukuwa uchaguzi bali ni mchezo wa kuigiza, ameendelea kuwa kwanza kulikuwa na wizi mkubwa ambapo wapiga kura hawakutumia hata kadi za uraia katika kutekeleza zoezi hilo.

Umoja wa Ulaya na Ubelgiji mkoloni wa zamani wa Burundi ambae pia ni mfadhili mkubwa wa serikali, wamebaini maskito yao kuona serikali imeendelea kuziba maskio na kushindwa kutekeleza ushauri kutoka jumuiya ya kimataifa na za kikanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.