Pata taarifa kuu
Nigeria-Boko haram-Jeshi-Usalama

Nigeria : jeshi laendesha mashambulizi dhidi ya Boko Haram

Jeshi la Nigeria limeendesha Jumatatu wiki hii mashambulizi ya anga katika vijiji vya Duwu, Jarawa, Mallum Maja na Mudu. Mashambulizi hayo yameendeshwa didi ya wapiganaji wa Boko Haram.

Jeshi la Nigeria laendesha mashambulizi ya anga dhidi ya Boko Haram.
Jeshi la Nigeria laendesha mashambulizi ya anga dhidi ya Boko Haram. Ben Shemang / RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwa miezi miwili sasa, wapiganaji wa Boko Haram wameingia kwa wingi katika wilaya ya Kalabalge ambapo vinapatikana vijiji vinne viliyoshambuliwa. Wapiganaji wa Boko Haram walitimuliwa hivi karibuni katika ngome zao kadhaa ziliyojimbo la Borno, ikiwa ni pamoja na miji ya Gwoza na Bama.

Kabla ya kuwasili kwa wapiganaji wa kundi hilo, maelfu ya raia wa Wilaya ya Kalabalge walikimbilia nchini Cameroon na Chad, zaidi ya kilomita kumi na mbili mashariki mwa Nigeria.

Lakini wapiganaji wa Boko Haram waliwakataza hivi karibuni raia kutoikimbia wilaya hiyo ili waweze kuwatumia kama ngao, kwa mujibu wa shahidi mmoja aliyehojiwa na shirika la habari la Ufaransa AFP, kabla ya kuongeza kuwa wapiganaji wa Boko Haram walikabiliwa na ukosefu wavifaa vya kutosha na kuamua kutumia pinde au mapanga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.