Pata taarifa kuu
Nigeria-Boko haram-Jeshi-Usalama

Nigeria: wanajeshi wakabiliwa na kesi za ukosefu wa nidhamu

Nchini Nigeria, jeshi limesema wanajeshi 579 na maaofisa wengine wa usalama wanakabiliwa na kesi za ukosefu wa nidhamu.

Wanajeshi wa Nigeria kwenye barabara inayoelekea Chibok, Kaskazini mashariki mwa Nigeria, Machi 5 mwaka 2015.
Wanajeshi wa Nigeria kwenye barabara inayoelekea Chibok, Kaskazini mashariki mwa Nigeria, Machi 5 mwaka 2015. AFP PHOTO/SUNDAY AGHAEZE
Matangazo ya kibiashara

Takwimu hizi zimetolewa baada ya wanajeshi 66 kuhukumiwa kunyongwa mwaka uliopita kwa kosa la kuisalliti serikali.

Ripoti zinasema kuwa wanajeshi wengi Kaskazini mwa nchi hiyo wamekuwa wakiakataa kufuata maagizo ya kukabiliana na Boko Haram kwa madai kuwa hawana silaha za kutisha na za kisasa kukabiliana na wanagambo hao.

Hivi karibuni maafisa wakuu wa jeshi la Nigeria wamesema jeshi la nchi hiyo limewaokoa wasichana wasiopungua 200 na kinamama wapatao 93 kutoka kambi ya Boko Haram ipatikanayo kwenye msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.