Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Nigeria: jeshi lawaokoa wanawake na wasichana zaidi ya 200

Maafisa wakuu wa Jeshi la Nigeria wamesema jeshi la nchi hiyo limewaokoa wasichana wasiopungua 200 na kinamama wapatao 93 kutoka kambi ya Boko Haram ipatikanayo kwenye msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Des militaires nigérians se préparent à une patrouille nocturne dans la forêt de Sambisa, fief de Boko Haram en avril 2014.
Des militaires nigérians se préparent à une patrouille nocturne dans la forêt de Sambisa, fief de Boko Haram en avril 2014. Ben Shemang / RFI
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Jeshi hilo Sani Oussmane, amesema watoto hao wa kike waliookolewa si miongoni mwa wale waliotekwa mwaka mmoja uliopita na kundi la kiislamu katika eneo la Chibok.

Amesema kwamba wanawake na watoto hao wa kike walikutwa katika kambi nne tofauti ambapo silaha pia zimekamatwa, baada ya kuziharibu kambi hizo.
Hata hivyo Olukolade amejizuia kutoa utambulisho wa wasichana hao.

Katika tangazo liliyorushwa hewani kwenye mtandao wa Twitter Jumanne Jioni, jeshi la Nigeria limetangaza kwamba limewaokoa angalau wasichana 200 na wanawake 93. Kuokolewa kwa watu hao kunakwenda sambamba na operesheni ya jeshi dhidi ya makambi ya Boko Haram katika msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.