Pata taarifa kuu
NIGERIA-UCHAGUZI-SIASA

Kampeni za uchaguzi za tamatika Nigeria

Saa chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Nigeria mwishoni mwa juma hili, wagombea wa kiti cha urais nchini humo wanatarajiwa kutamatisha kampeni zao leo ijumaa.

Mkutano wa chama cha PDP, ukiongozwa na Rais anayemaliza muda wake Goodluck Jonathan, katika mkoa wa Akwa Ibom, katikati ya mwezi Machi mwaka 2015.
Mkutano wa chama cha PDP, ukiongozwa na Rais anayemaliza muda wake Goodluck Jonathan, katika mkoa wa Akwa Ibom, katikati ya mwezi Machi mwaka 2015. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wakati huohuo chuano mkali unatarajiwa kuwa kati ya rais Goodluck Jonathan na kiongozi wa upinzani, Muhammadu Buhari.

Uchaguzi mkuu nchini Nigeria unatarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii baada ya kuahirishwa mwezi February kutokana na sababu za kiusalama, uchaguzi ambao wachambuzi wa mambo wanasema utakuwa wa upinzani mkali kati ya wagombea wawili, rais anaye maliza muda wake Goodluck Jonathan na mpinzani wake Muhammadu Buhari.

Njia za barabara na mipaka ya bahari ya Nigeria imefungwa toka usiku wa Jumatano kwa lengo la kuhakikisha kila anaeingia kwenye maeneo ya mipaka anakaguliwa na vyombo vya usalama ikiwa ni pamoja na kuweka muda maalumu wa kutembea.

Nchi ya Nigeria imekuwa ikikumbwa na machafuko ya wakati na baada ya uchaguzi, lakini safari hii, rais Jonathan na mpinzani wake Buhari wameonesha nia ya wazi ya kuhakikisha wanawashawishi wafausi wao kutorudia makosa ya mwaka 2011 ambapo watu elfu 1 walipoteza maisha baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.

Licha ya tishio la mashambulizi ya kundi la Boko Haram, rais Jonathan na mwenzake Muhammadu Buhari mwezi January mwaka huu walitiliana saini mkataba wa kuheshimu matokeo ya urais kuepusha vurugu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.