Pata taarifa kuu
MAREKANI-NIGERIA-BOKO HARAM-SIASA

Marekani yatolea wito kwa wananchi wa Nigeria

Serikali ya Marekani imetoa wito kwa wananchi na wagombea wa kiti cha urais nchini Nigeria, kushiriki uchaguzi wa mwishoni mwa juma kwa amani ikiwa ni pamoja na kila upande kuepuka kuchochea vurugu wakati wa uchaguzi huu.

Rais wa Marekani Barack Obama awatolea wito raia na wagombea wa kiti cha urais nchini Nigeria, kushiriki uchaguzi wa mwishoni mwa juma kwa amani ikiwa ni pamoja na kila upande kuepuka kuchochea vurugu wakati wa uchaguzi.
Rais wa Marekani Barack Obama awatolea wito raia na wagombea wa kiti cha urais nchini Nigeria, kushiriki uchaguzi wa mwishoni mwa juma kwa amani ikiwa ni pamoja na kila upande kuepuka kuchochea vurugu wakati wa uchaguzi. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Akitoa ujumbe wake kuelekea uchaguzi mkuu nchini Nigeria, rais Barack Obama amewataka wagombea wote kuhakikisha wanawashawishi wananchi kutojihusisha na vurugu na kwamba uchaguzi uwe huru, wazi na haki.

Kwenye hotuba yake rais Obama amesema ili kundi la Boko Haram lidhibitiwe kutokana na mashambulizi yake, ni lazima wananchi waoneshe umoja kwa kuchagua kiongozi wanaemtaka kushughulikia masuala ya usalama.

Katika hatua nyingine polisi nchini Nigeria wametangaza kwa nyakati tofauti wakati wa zoezi la upigaji kura, kutakuwa na udhibiti wa magari yatakayoruhusiwa kuingia na kutoka kwenye baadhi ya miji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.