Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-SIASA

Burkina Faso: Serikali mpya ya mpito yatangazwa

Orodha ya mawaziri wanaounda serikali ya mpito nchini Burkina faso imejulikana tangu Jumapili Novemba 23 jioni baada ya kuchelewa kutangazwa kwa muda wa saa mbili. Serikali hiyo mpya ya mpito inaundwa na mawaziri 26, wengi wakiwa ni wanajeshi.

Waziri mkuu akiwa pia waziri wa ulinzi, luteni kanali Isaac Zida, Novemba 21 mwaka 2014.
Waziri mkuu akiwa pia waziri wa ulinzi, luteni kanali Isaac Zida, Novemba 21 mwaka 2014. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Sherehe za kukabidhiana madaraka kati ya rais wa mpito na waziri mkuu ziliendelea hadi Jumapili jioni Novemba 23. Serikali hiyo ya mpito inaundwa na idadi kubwa ya wanajeshi. Zida na Kafando, pamoja na majukumu yao ya sasa, wataendelea kushikia idara muhimu.

Tangazo hilo lilianza na hotuba fupi iliyotolewa na Isaac Zida. Waziri mkuu ameomba radhi kwa kuchelewa kiasi cha masaa mawili bila kutoa maelezo zaidi. Viongozi hao wawili wamesema kuwa wataonesha mfano mzuri katika majukumu yao. Rais Michel Kafando, mwanadiplomasia wa zamani, atashikilia wizara ya mambo ya nje. Kwa upande wake luteni kanali Zida, Waziri Mkuu, atashikilia wizara ya ulinzi. Uamuzi ambao umechukuliwa kupitia dikri mbili.

Waziri mkuu Isaac Zida ndiye atakua na jukumu la kufanya mageuzi katika jeshi, na hasa katika kikosi cha usalama wa rais. Kikosi ambacho kiliundwa ili kuhakikisha usalama wa rais wa zamani Blaise Compaoré. Wengi miongoni mwa wanajeshi wanaounda kikosi hicho majina yao yalitajwa katika mauaji ya mwandishi wa habari Norbert Zongo.

Mbali na luteni kanali Isaac Zida, wanajeshi wengine watatu wameteuliwa katika serikali hiyo. Wanajeshi hao ni Kanali Auguste Denise Barry, mmoja wa washirika wa karibu wa waziri mkuu, ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa utawala na usalama, sawa na wizara ya mambo ya ndani. Nafasi ambayo alihudumu mwaka 2011, kabla ya wimbi la maandamano lililoshufudiwa nchi nzima. Kanali Auguste Denise Barry atakua na jukumu la kuanzisha mfumo wa usalama wa matukio mbalimbali ya mashambulizi yanayoendeshwa na makundi yenye silaha na uhalifu uliyokithiri.

David Kabré, ambaye aliwakilisha jeshi katika mazungumzo ya mkataba wa mpito, ameteuliwa kuwa waziri wa michezo. Wizara ya madini na nishati imekabidhiwa Kanali Boubacar Ba. Kwa kipindi kirefu Bukina Faso ilichukuliwa kama nchi ya kilimo, lakini kwa sasa imechukua nafasi nzuri kama nchi ya madini. " Kuanzia mwaka 2015, Burkina Faso itakua na migodi kumi ya dhahabu. Kufuatia hali hiyo, uzalishaji utaongezeka kutoka tani 32 hadi 40", alielezea Waziri wa zamani wa madini na nishati. Mashirika ya kiraia yaliwahi kuzindua kampeni ya utetezi kudai "asilimia 1 ya fedha za dhahabu kuinua jumuiya kutoka katika umaskini".

Waziri wa mawasiliano, akiwa pia msemaji wa serikali ya mpito ni Frédéric Nikiema. Loada Augustin ambaye ni maarufu nchini Burkina Faso, ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa Kituo kwa minajili ya Utawala wa Kidemokrasia. Ni anapata Wizara ya Kazi. Hatimaye, mwanaharakati Josephine Ouedraogo, ambaye alikuwa akigombea urais, ameteuliwa kuwa waziri wa sheria. Wanachama wengi wa serikali hiyo ya mpito karibu wote hawajulikani, na huenda wakajulikana Jumatatu wiki hii. Mkutano wa kwanza wa Baraza jipya la mawaziri unatazamiwa kufanyika leo Jumatatu Novemba 24.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.