Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Blaise Compaoré aondoka Côte d'Ivoire

Aliyekuwa rais wa Bukina Faso, Blaise Compaoré ameondoka Côte d'Ivoire na kujielekeza Morocco. Blaise Compaoré ameondoka na familia yake, Ikulu ya Abidjan imethibitisha.

Blaise Compaoré, aliyekuwa rais wa Burkina Faso, ameondoka Côte d'Ivoire .
Blaise Compaoré, aliyekuwa rais wa Burkina Faso, ameondoka Côte d'Ivoire . REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Blaise Compaoré alikimbilia Yamoussoukro Oktoba 31, siku alipojiuzulu. Ikulu ya Abidjan imesema Blaise Compaoré anaruhusiwa kuingia na kutoka katika aridhi ya Côte d'Ivoire.

Luteni kanali Isaac Zida ateuliwa kuwa Waziri mkuu, Ouagadougou, Burkina Faso, Novemba 14 mwaka 2014.
Luteni kanali Isaac Zida ateuliwa kuwa Waziri mkuu, Ouagadougou, Burkina Faso, Novemba 14 mwaka 2014. ISSOUF SANOG / AFP

Mapema Jumatano jioni Novemba 19, chama cha CDP cha Blaise Compaoré kiliomba radhi kwa kukosa kubwa kiliyofanya la kutaka kufanya marekebisho ya Katiba, jambo ambalo lilizua maandamano na ghasia hadi kupelekea rais Blaise Comaporé kujiuzulu, na kukimbilia katika mji wa Yamoussoukro nchini Côte d'Ivoire

Wakati huohuo rais wa mpito wa Burkina Faso, Michel Kafando amemteua Jumatano Novemba 19 luteni kanali Isaac Zida kuwa Waziri mkuu.
Awali luteni kanali Yacouba Isaac Zida alisema yuko tayari kushikilia wadhifa wa Waziri mkuu iwapo atateuliwa.

Luteni kanali Yacouba Isaac Zida anatazamiwa kwa upande wake kuunda baraza la mawaziri 25 ndani ya saa 72, kukabiliana na changamoto ambazo rais wa mpito, Michel Kafando, alizibainisha siku ya Jumanne Novemba 18 wakati wa kuapishwa kwake na ambaye anatumaini kuwa wananchi wa Burkina Faso watachangia kikamilifu kutatua matatizo hayo.

Uteuzi wa luteni kanali Yacouba Isaac Zida umezua hisia tafauti, baadhi wamekaribisha uteuzi huo, huku wengine wakiwemo baadhi ya wanadiplomasia wa kigeni wakipinga kuona mwanajeshi akishikilia wadhifa wa Waziri mkuu.

Rais wa mpito, Michel Kafando aliteuliwa Jumanne Novemba 18 kuwa rais kwa muda wa mwaka mmoja, kupitia makubaliano yaliyoafikiwa na wadau wote katika mgogoro uliyokua ukiendelea nchini Burkina Faso, baada ya maandamano ya raia kuangusha utawala wa Blaise Compaoré.

" Nataka kuwaambia kwamba nimepokea majukumu haya kwa heshima kubwa, lakini pia kwa unyenyekevu mkubwa", rais mpya wa mpito alisema katika hotuba yake ya kwanza aliyoitoa Jumanne Novemba 18. Rais Michel Kafando aliongeza kwamba "unyenyekevu wa mtu unaonekana pale anapoheshimu muda wa madaraka anaopewa kwa kipindi cha mpito, unyenyekevu wa mtu pia ni kufahamu kwamba cheo ni dhamana".

Rais wa mpito wa Burkina Faso, Michel Kafando anatazamiwa kukabidhiwa rasmi madaraka ya uongozi wa nchi Ijumaa Novemba 21.
Rais wa mpito wa Burkina Faso, Michel Kafando anatazamiwa kukabidhiwa rasmi madaraka ya uongozi wa nchi Ijumaa Novemba 21. AFP/Romaric Hien

Blaise Compaoré, alitimuliwa madarakani, alipokua akijaribu kufanya marekebisho ya Katiba ili aweze kugombea muhula mwengine, baada ya kuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 27.

Luteni kanali Yacouba Isaac Zida alichukua madaraka ya uongozi wa nchi, baada ya Blaise Compaoré kutimuliwa madarakani. Hata hivo hali hiyo iliendelea kuzua mvutano, huku raia wakiendelea kuandamana, wakiomba jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.

Rais wa mpito Michel Kafando aliapishwa Jumanne Novemba 18, na anatazamiwa kukabidhiwa rasmi madaraka ya uongozi wa nchi Ijumaa Novemba 21, na kutamatisha moja kwa moja utawala wa kijeshi ulioongoza taifa hilo kwa muda wa siku 16.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.