Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: Maandalizi ya kuapishwa kwa rais mpya

Rais wa mpito nchini Burkina faso, Michel Kafando, anatarajiwa kuapishwa leo Jumanne Novemba 18, kabla ya kukabidhiwa Ofisi na Luteni Kanali Isaac Zida Ijumaa Novemba 21 katika sherehe maalum itakayohudhuriwa na marais kadhaa wa Ukanda wa nchi za Afrika Magharibi. 

Kaimu rais wa Burkina Faso, Michel Kafando, Ouagadougou, Novemba 17 mwaka 2014.
Kaimu rais wa Burkina Faso, Michel Kafando, Ouagadougou, Novemba 17 mwaka 2014. AFP/ROMARIC HIEN
Matangazo ya kibiashara

Kati ya marais wanaotarajiwa kuanza kuwasili nchini humo ni pamoja na rais wa Ghana, rais wa Senegal, wa Togo na wa Mauritania ambao ni wasuluhishi katika majadiliano ya nchini Burkina Faso, lakini pia marais wa Mali na Niger.

Uteuzi wa Michel Kafando utasahihishwa na Korti ya kikatiba, na kupelekea kutamatika kwa utawala wa kijeshi uliyoongoza nchi hiyo kwa kipindi cha siku kumi na sita, baada ya kuangushwa utawala wa Blaise Compaoré. Wakati huohuo mchakato wa taasisi za mpito utaendelea kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi utakapofanyika uchaguzi wa urais na wa wabunge.

Umoja wa Afrika, Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na Ufaransa vimepongeza kurejea kwa utawala wa kiraia nchini Burkina Faso.

Rais mteule Michel Kafando, anatazamiwa kula kiapo mbele ya Wazee wa Busara, ambao wanawakilisha kwa sasa makundi mbalimbali ya raia wa Burkina Faso.

Sherehe hizi ni muhimu, kwani zintampa nafasi rais huyo mteule kuanza majukumu ya urais yanayo msubiri. Uteuzi wa Waziri mkuu unatazamiwa kufanyika Jumatano Novemba 19, na Alhamisi Novemba 20 itatangazwa serikali mpya yenye wajumbe 25.

Sherehe za kukabidhiana madaraka zitafanyika Ijumaa Novemba 21 kati ya rais mteuke, Michel Kafando, na luteni kanali,Yacouba Isaac Zida, aliyepitishwa na jeshi kuchukua madaraka ya uongozi wa nchi baada ya maandamano ya raia kuangusha utawala wa Blaise Compaoré.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.