Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: mkataba wa mpito watazamiwa kutiliwa saini Jumapili hii

Zoezi la kutia saini kwenye mkataba wa mpito utakaopelekea kuundwa kwa taasisi za uongozi wa nchi, Burkina Faso, ambao ambalolimekua limepangwa kufanyika Jumamosi hii, limeahirishwa hadi kesho Jumapili Novemba. 

Luteni kanali Isaac Zida, Ouagadougou Novemba 2 mwaka 2014.
Luteni kanali Isaac Zida, Ouagadougou Novemba 2 mwaka 2014. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Luteni kanali Yacouba Isaac Zida aliyepitishwa na jeshi kwenye uongozi wa nchi, Burkina Faso, Ijumaa alaasiri Novemba 14 aliwapokea wajumbe wa vyama vya kiraia, vyama vya upinzani, pamoja na viongozi wa kidini.

Wajumbe hao walikua wamekuja kurejesha toleo la mwisho la mkataba wa mpito ambao ulisahihishwa Alhamisi Jioni Novemba 13 mwaka 2014.

Mkataba wa mpito ulipitishwa na wadau wote walioshiriki mazungumzo, ikiwa ni pamoja na wanasiasa, wajumbe wa vyama vya kiraia, wanajeshi pamoja na viongozi wa kidini na kimila.Hata hivyo wadau hao hawajatia saini kwenye mkataba huo. Tangazo lilitolewa na wawakilishi wa pande zote husika katika mgogoro huo.

Wajumbe 150 kutoka makundi mbalimbali ndio walishiriki katika mazungumzo hayo yaliyopelekea kupatikana kwa mkataba huo wa mpito, utaopelekea kuundwa kwa taasisi za mpito za uongozi wa nchi.

“ Kazi muhimu tumemaliza, hatua inayofuata ni kutia saini kwenye mkataba wa mpito”, Zéphirin Diabré.

Awali Jeshi lilisema kuridhishwa na hatua hiyo iliyofikiwa. “ Kwa kweli tumeridhishwa na jinsi mazungumzo yalivyoendeshwa, kwa hiyo kazi kubwa imekamilika”, amesema, David Kabré, mmoja kati wajumbe wa jeshi waliyoshiriki katika mazungumzo hayo.

Hati ya mwisho atakabidhiwa luteni kanali Zida ambaye atarejesha Katiba ili kuruhusu wajumbe kutoka makundi yote yaliyoshiriki mazungumzo, kutia saini kwenye mkataba wa mpito.

Mara tu baada ya mkataba kusainiwa, hatua ya kwanza itakayofuata ni mchakato wa kuteua rais wa mpito. Rais huyu atateuliwa kutoka vyama vya kiraia. Rais huyo mteule atamteua kwa upande wake waziri mkuu ambaye huenda akawa ni mwanajeshi. Waziri mkuu kwa upande wake atakua na majukumu ya kuunda serikali yenye mawaziri 25.

Wakati huohuo Baraza la kitaifa la mpito au Bunge, litaundwa. Taasisi hii ni muhimu hasa kwa upande wa vyama vya kiraia. Baraza hilo la kitaifa la mpito litakua na wajumbe 90. Upinzani utakua na wajumbe 30, jeshi litawakilishwa na wajumbe 25, vyama vya kiraia vitakua na wajumbe 25 na vyama viliyokua na uhusiano wa karibu na chama tawala cha zamani cha Blaise Compaore vitakua na wajumbe 10.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.