Burkina Faso: Michel Kafando ateuliwa kuwa rais wa mpito
Baada ya kucheleweshwa kwa siku moja kutokana na matatizo ya kiufundi na vifaa, mkataba wa mpito ulisainiwa siku ya Jumapili Novemba 16 katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, na vikosi vya ulinzi na usalama, vyama vya siasa, viongozi wa dini pamoja na vyama vya kiraia.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Mapema Jumatatu Novemba 17 asubuhi, mwanadiplomasia Michel Kafando ameteuliwa kuwa rais wa mpito wa Burkina Faso.
Ni rasmi sasa, mkataba wa mpito, ambao utasaidia kuzindua shughuli za taasisi za mpito, ulisainiwa kwa vifijo na nderemo na wadau wote waliochangia kwa kupatikana suluhu katika mgogoro uliyokua ukiendelea nchini Burkina Faso.
Watu kutoka makundi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama,vyama vya siasa, vyama vya kiraia, viongozi wa kidini na kimila.
Vifijo na nderemo vilisikika wakati Luteni Kanali Zida alipoinua mikono yake iliyokua ikishikilia nakala ya mkataba huo uliyosaniwa. Kiongozi wa upinzani, Zephyrinus Diabré, Amadou Dabo, mbunge wa zamani wa chama tawala cha Blaise Compaoré, mwanasheria Luc Marius Ibriga ambae amekua akiwakilisha vyama vya kiraia pamoja na padri Henri Yé, aliye wakilisha dini wamepongeza hatua hiyo.
Michel Kafando, mwenye umri wa miaka 72 aliwahi kuwa balozi wa Haute-Volta katika miaka ya 1980, na baadae balozi wa Burkina Faso kati ya miaka 1998 na 2011. Wagombea wengine wawili waliokua katika kinyanganiro hicho ni Joséphine Ouedraogo, waziri wa zamani katika utawala wa thomas Sankara, pamoja na mwandishi wa habari Cherif Sy.