Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: rais mpya Michel Kafando aapishwa

Mwanadiplomasia wa zamani, Michel Kafando, aliyeteuliwa hivi karibuni kwa makubaliano ya wadau wote katika mgogoro uliyokua ukiripotiwa nchini Burkina Faso kuwa rais wa mpito, ameapishwa leo Jumanne Novemba 18 asubuhi.  

Rais wa mpito wa Burkina Faso, Michel Kafando aanza majukumu ya urais baada ya kuapishwa mbele ya jopu la Wazee wa Busara, Novemba 18 mwaka 2014.
Rais wa mpito wa Burkina Faso, Michel Kafando aanza majukumu ya urais baada ya kuapishwa mbele ya jopu la Wazee wa Busara, Novemba 18 mwaka 2014. AFP/ROMARIC HIEN
Matangazo ya kibiashara

Sherehe za kuapishwa kwa rais wa mpito Michel Kafando zimetamatisha utawala wa kijeshi uliyoongoza nchi kwa kipindi cha siku 16 baada ya maandamano ya raia yaliyouwangusha utawala wa Blaise Compaoré aliyoongoza taifa hilo kwa kipindi cha miaka 27.

Michel Kafando atakabidhiwa rasmi madaraka Ijumaa Novemba 21, na atashikilia madaraka hayo kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi utakapofanyika uchaguzi mkuu wa rais na wa wabunge mwezi Novemba mwaka 2015.

" Nataka kuwaambia kwamba nimepokea majukumu haya kwa heshima kubwa, lakini pia kwa unyenyekevu mkubwa", rais mpya wa mpito amesema katika hotuba yake ya kwanza. Rais Michel Kafando ameongeza kwamba "unyenyekevu wa mtu unaonekana pale anapoheshimu muda wa madaraka anaopewa kwa kipindi cha mpito, unyenyekevu wa mtu pia ni kufahamu kwamba cheo ni dhamana".

Sherehe za kuapishwa kwa rais huyo wa mpito zimefanyika katika mazingira mazuri, huku hotuba yake ikidumu dakika nne tu, akiwataka raia wake kuwa na heshima na maadili na kuwa pia na wajibu wa kwenda mbele.

Uteuzi wa Waziri mkuu unatazamiwa kufanyika Jumatano Novemba 19, na Alhamisi Novemba 20 itatangazwa serikali mpya yenye wajumbe 25. Hata hivyo luteni kanali Yacouba Isaac Zida amesema yuko tayari kushikilia wadhifa wa Waziri mkuu iwapo atateuliwa. Kulingana na mkataba wa mpito, anaweza akateuliwa kwenye wadhifa wa Waziri mkuu raia wa kawaida au mwanajeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.