Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: rais wa mpito Michel Kafando awasili rasmi ikulu ya Kossyam

Wakati serikali mpya ikisubiriwa kutangazwa nchini Burkina Faso, sherehe kubwa ya kumkabidhi madaraka ya uongozi wa nchi rais wa mpito Michel Kafando inatazamiwa kufanyika leo Ijumaa jioni Novemba 21.

Rais wa mpito wa Burkina Faso, Michel Kafando wakati wa kuapishwa kwake mjini Ouagadougou, Novemba 18 mwaka 2014.
Rais wa mpito wa Burkina Faso, Michel Kafando wakati wa kuapishwa kwake mjini Ouagadougou, Novemba 18 mwaka 2014. AFP PHOTO / ROMARIC HIEN
Matangazo ya kibiashara

Sherehe hiyo itafanyika katika Jumba la michezo mjini Ouagadougou, sherehe ambayo ni ya kihistoria itakayohudhuriwa na marais pamoja na viongozi wengine wengi kutoka ukanda wa Afrika Magharibi.

Viongozi ambao wamethibitisha kuwa watahudhuria katika sherehe hiyo ni pamoja na marais wa Ghana, Togo, Mauritania, Senegal, Mali na Niger, na inatazamiwa kuwa huenda marais hao wakajieleza kuhusu somo walilopata kufuatia tukio la kuangushwa kwa utawala wa Blaise Compaoré ambae alitaka kung'ang'ania madarakani, baada ya kuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 27.

Inaarifiwa kuwa rais wa Cote d'Ivoire, Alassane Ouattara hatahudhuria sherehe hiyo, na huenda akawakilishwa na Waziri wake wa mambo ya nje.

Hayo yanajiri wakati aliyekuwa rais wa Burkina Faso, Blaise Compaoré amewasili Morocco akitokea Côte d'Ivoire Alhamisi Novemba 20. Ikulu ya Côte d'Ivoire imeiambia RFI kwamba rais huyo wa zamani wa Burkina faso amejielekeza Morocco kwa mwaliko wa Mfalme wa taifa hilo, Mohammed 6.

Blaise Compaoré amekua akiishi katika mji wa Yamoussoukro, baada ya kujiuzulu Oktoba 31 mwaka 2014 kufuatia maandamano ya raia yaliyoitishwa na upinzani pamoja na vyama vya kiraia.

Morocco imejizuia kutoa taarifa yoyote kuhusu sehemu sahihi aliko na muda gani ataishi nchini humo.

Kuondoka kwa Blaise Compaoré nchini Côte d'Ivoire kumezua hisia tofauti katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.