Pata taarifa kuu
AFRIKA-CAF-QATAR-SOKA-MICHEZO

Soka: Qatar iko tayari kusaidia maandalizi ya ACN 2015

Shirikisho la soka la Qatar limesema liko tayari kusimamia maandalizi ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika itakayochezwa kuanzia Januari 17 hadi Februari 8 mwaka 2015, iwapo viongozi wa Emirate watafahamishwa rasmi, amesema Alhamisi Novemba 13 rais wa shirikisho hilo.

Wachezaji wa timu ya soka ya Qatar, wakiimba wimbo wa taifa.
Wachezaji wa timu ya soka ya Qatar, wakiimba wimbo wa taifa. REUTERS/Soe Zeya Tun
Matangazo ya kibiashara

Cheikh Hamad Ben Khalifa Ben Ahmed Al Thani amepingana na naibu wake, ambaye alisema Jumatano wiki hii kwamba michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kuchezwa nje ya Afrika itakua haina “umuhimu wowote”.

Qatar imebaini kwamba iko tayari kua mwenyeji wa michuanao ya kombe la mataifa barani Afrika. Uamzi huo unakuja baada ya mataifa zaidi ya tano kutoka barani Afrika kukataa kusimamia maandalizi ya michuano hiyo yakidai kkuhofia afya ya raia wao.

Morocco Ambayo ingelikua mwenyeji wa michuano hiyo iliomba iahirishwe kufuatia mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola, lakini shirikisho la soka barani Afrika CAF pamoja na shirikisho la soka dunia FIFA, vilitupilia mbali hoja hiyo.

Ikiwa michuano hiyo itachezwa Qatar, itakua mara ya kwanza michuano ya kombe la mataifa ya Afrika inachezwa nje ya Afrika.

Rais wa shirikisho la soka la Qatar cheikh Hamad Ben Khalifa Ben Ahmed Al Thani, amesema hawakupata ombi rasmi kwa minajili ya maandalizi ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015.

“ Kwa sasa uamzi utachukuliwa na CAF”, amesema cheikh Hamad Ben Khalifa Ben Ahmed Al Thani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.