Pata taarifa kuu
AFRIKA-MOROCCO-CAF-SOKA-MICHEZO

Morocco yajiondoa kuwa mwenyeji wa michuano ya kuwania taji la timu bora

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limethibitisha kuwa nchi ya Morroco haitakuwa mwenyeji wa michuano ya kuwania taji la timu bora barani Afrika mwaka ujao.

Timu ya Morocco inashangilia baada ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la mataifa Afrika ANC 2012.
Timu ya Morocco inashangilia baada ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la mataifa Afrika ANC 2012. Reuters
Matangazo ya kibiashara

CAF imesema, Morroco imejiondoa kutokana na hofu kuwa ugonjwa hatari wa Ebola huenda ukafika nchini humo ikiwa michuano hiyo itaendelea kama ilivyopangwa kufanyika kati ya Januari tarehe 17 hadi tarehe 8 mwezi Februari mwakani.

Hata hivyo, CAF haijatangaza ni nchi gani itachukua nafasi ya Morroco lakini viongozi wa Shirikisho hilo ambao wamekutana jijini Cairo Misri wamesisitiza kuwa michuano hiyo itaendelea kama ilivyopangwa.

Aidha, uongozi huo umesema tayari umepata maombi kutoka mataifa kadhaa kutaka kuwa wenyeji wa michuano hiyo na mwenyeji atatangazwa baadaye.

CAF imeiondoa Morroco kushiriki katika michuano ya mwaka ujao,na walikuwa wamepewa hadi jumamosi iliyopita kuthibitisha ikiwa watakuwa wenyeji au la.

Morroco ilikuwa imeomba michuano hiyo kuahirishwa kwa muda wa mwaka mmoja kwa hofu ya Ugonjwa huo, ombi ambalo CAF ilikataa.

Michuano ya mwisho kufuzu katika fainali hizo zilipangwa kufanyika mwishoni mwa juma hili, itaendelea kama ilivyopangwa na CAF imesema kuwa, droo ya timu zitakazokuwa zimefuzu itafanyika tarehe 14 au 15 kama ilivyoratibiwa.

Ghana na Afrika Kusini zilikuwa zimetajwa huenda zikachukua nafasi ya Morroco lakini, viongozi wa vyama vya soka nchini humo wamekanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.