Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: upinzani na vyama vya kiraia vyasahihisha "mkataba" wao

Kukamilika kwa rasimu ya mkataba ya mpito kumepelekea upinzani na vyama vya kiraia nchini Burkina Faso kuafikiana kuhusu baadhi ya vifungu hususan kugawana madaraka katika taasisi mbalimbali za uongozi wa nchi.

Vyama vya siasa vya upinzani, vyama vya kiraia, viongozi wa dini na kimila walikutana na kupitisha kwa pamoja mkataba wa taasisi za mpito, Burkina Faso Novemba 8, 2014.
Vyama vya siasa vya upinzani, vyama vya kiraia, viongozi wa dini na kimila walikutana na kupitisha kwa pamoja mkataba wa taasisi za mpito, Burkina Faso Novemba 8, 2014. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Rasimu ya mkataba huo iliyopitishwa bila kupingwa imependekeza kuundwa kwa serikali mpya itakayo kuwa na wajumbe 25 kufuatia hgali inayojiri wakati huu nchini Burkina Faso.

Wajumbe kutoka vyama vya siasa, vyama vya kiraia, viongozi mbalimbali wa kidini na viongozi wa kimila wameafikiana kuundwa kwa serikali hiyo mpya itakayojumuisha pande zote husika katika mgogoro unaoendelea nchini humo.

Bunge litaundwa na Wabunge zaidi ya 100. Bunge hilo litaundwa kwa kuzingatia vyama viliyokua karibu na utawala wa zamani wa Blaise Compaoré. Upinzani utapata viti 40, vyama vya kiraia vitakua na viti 30, jeshi litakua na viti10 pamoja vyama vingine vya saiasa visiyoegemea upande wowote vitapata viti 10.

Wajumbe wote wa Bunge la mpito wanaweza kugombea katika chaguzi zijazo. Hata hivyo rais pamoja, waziri mkuu na wajumbe wa serikali ya mpito hawataweza kugombea katika chaguzi zijazo, ambazo zitafanyika baada ya serikali ya mpito.

Ili kuepuka mgogoro mwingine kama ule uliyotokea kutokana na jaribio la marekebisho ya Katiba, wajumbe walioshiriki mazungumzo hayo waliafikiana kuweka sawa baadhi ya vifungu : "Ibara ya 4 ya rasimu ya mkataba inasema rais wa mpito haruhusiwi kugombea katika cghaguzi zijazo baada ya serikali ya mpito, yaani uchaguzi wa Wabunge na urais ambao utakamilisha kipindi cha mpito. Tumeafikiana kwamba Ibara hii haipaswi kufanyiwa marekebisho", amesema Luc Marius Ibriga, kiongozi wa shirika la kiraia (Focal) akiwa pia profesa wa sheria ya katiba, kabla ya kusisitiza: "Tumechukua tahadhari ya kuizuia Ibara hiyo ili rais yeyote atakaye kuja baadae asiwezi kuifanyia marekebisho kwa lengo la kugombea katika uchaguzi mwengine".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.