Pata taarifa kuu
MALI-UN-Usalama

Mali: kambi ya UN (Minusma) yashambuliwa

Kambi ya Umoja wa Mataifa nchini Mali iliyoko katika mji wa Aguelhoc, imeshambuliwa kwa roketi karibu na mpaka na Algeria. Kambi hiyo ilishambuliwa kwa roketi siku mbili ziliyopita, amesema mkuu wa polisi wa Somalia.

Wapiganaji wa MNLA, katika mji wa Kidal.
Wapiganaji wa MNLA, katika mji wa Kidal. AFP PHOTO / MNLA
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni kambi hiyo imeshambuliwa kwa roket 4 mapema ijumaa asubuhi wiki hii, ameendelea kusema mkuu huo wa polisi , bila hata hivo kutobaini iwapo kuna hasara iliyosababishwa na mashambulizi hayo.

Mwanamgambo mmoja wa kiislamu aliye na ushirikiano wa karibu na kundi la Mujao amekiri jumatatu wiki hii kwamba wamehusika na mashambulizi hayo dhidi ya kambi ya Umoja wa Mataifa, inayopatikana katika jimbo la Kidal.

“Kwa jina la wanajihadi wote, tumeendesha mapema ijumaa wiki hii mashambulizi dhidi ya kambi ya maadui wa Uislam katika mji wa Aguelhoc, Sultan Ould Bady, ameliambia kwa simu shirika la habari la Ufaransa AFP.

Ramani ya operesheni za Minusma nchini Mali, mji wa Aguelhok ukiwa ndio unalengwa..
Ramani ya operesheni za Minusma nchini Mali, mji wa Aguelhok ukiwa ndio unalengwa.. RFI/http://www.un.org/Depts/Cartographic/map/dpko/MINUSMA.pdf

Kwa mujibu wa chanzo cha ofisi ya Umoja wa Mataifa, roketi moja miongoni mwa 9 ziliyorushwa dhidi ya kambi hiyo ndio imedondoka ndani ya kambi, bila hata hivo kusababisha hasara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.