Pata taarifa kuu
UFARANSA-ALGERIA-MALI-Ajali ya ndege-Usalama wa anga

Uchunguzi unaendelea kuhusu ajali ya ndege ya Air Algeria

Bawa la ndege ya shrika la ndge ya Algeria “Air Algerie” limepatikana kwenye umbali wa kilomita 100 kusini magharibi mwa mji wa Gao, ambako ni kaskazini mwa Mali, karibu na mpaka na Burkina Faso.

Uchunguzi kuhusi ajali ya ndege ya shirika la ndege la Uhispania iliyokodiwa na shirika la ndege la Algeria unaendelea.
Uchunguzi kuhusi ajali ya ndege ya shirika la ndege la Uhispania iliyokodiwa na shirika la ndege la Algeria unaendelea. REUTERS/Lennart Boettcher
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo imepata ajali alhamisi wiki hii ikiwa na abiria 118. Kisanduku cha sauti kimepatikana na kinasubiri kusafirishwa katikajimbo la Gao, nchini Mali.

Wanajeshi wa Ufaransa wametumwa kwenye eneo la tukiyo ili kulinda eneo hilo. “Bado haijafahamika chanzo cha ajali”, amesema waziri wa Ufaransa mwenye dhamana ya mambo ya nje, Laurent Fabius.

Ndege hiyo yenye chapa AH 5017 ya shirika la ndege la Algeria, imekua ikifanya safari zake Ouagadougou-Alger mara nne kwa wiki. Hapo jumatano kabla ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa nchini Burkina Faso, ilikua ilifanya safari ya nenda-rudi Paris kuelekea mji wa Batna, kusini mashariki mwa Algeria.

Kwa mujibu wa duru za kuaminika, ndege hiyo iliondoka kwenye uwanja wa ndege wa Ougadougou ikipaa angani saa sita na dakika 17 usiku saa za kimataifa, wala siyo saa saba na dakika tano usiku kama ilivyotangazwa hapo awali. Na ingeliwasili mjini Algiers, nchini Algeria saa kumi na dakika 40 alfajiri saa za kimataifa.

Ndege hiyo ilipoteza mawasiliano muda mchache ilipopaa angani ikitokea kwenye uwanja wa ndege wa Ouagadougou saa saba na dakika 38 usiku saa za kimataifa

Ndege hiyo iliyopata ajali ni ya shirika la ndege la Uhispania Swiftair, ambayo ilikua ilikodiwa na shirika la ndege la Algeria “air Algerie”, na ilikua na miaka 18 ikifanya usafiri wa angani.

Ndege hiyo ya Algeria “Air Algerie” chapa AH 5017 ilipata ajali ikiwa na abiria 118 hususan raia 51 wa Ufaransa, raia 28 kutoka Burkina Faso, kwa mujibu wa viongozi wa Burkina Faso na wengine kutoka. Walikuemo pia raia kutoka mataifa malimbali, Canada, Libanon, Algeria. Watu sita wengine ambao ni marubani , mafundi na wasaidizi wengine ni kutoka Uhispania.

Kwa mujibu wa majeshi ya Ufaransa hakuna mtu alienusurika katika ajali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.