Pata taarifa kuu
UFARANSA-ALGERIA-MALI-Ajali ya ndege-Usalama wa anga

Ajali ya ndege ya Algeria yaendelea kuzua msisimko

Bawa la ndege ya shrika la ndge ya Algeria “Air Algerie” limepatikana kwenye umbali wa kilomita 100 kusini magharibi mwa mji wa Gao, ambako ni kaskazini mwa Mali, karibu na mpaka na Burkina Faso. Ndege hiyo imepata ajali alhamisi wiki hii ikiwa na abiria 116.

Ndege ya Algeria iliyopata ajali kitokea Burkina Faso ikielekea Algeria.
Ndege ya Algeria iliyopata ajali kitokea Burkina Faso ikielekea Algeria. ©REUTERS/Xavier Larrosa
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wa Ufaransa wametumwa kwenye eneo la tukiyo ili kulinda eneo hilo. “Bado haijafahamika chanzo cha ajali”, amesema waziri wa Ufaransa mwenye dhamana ya mambo ya nje, Laurent Fabius.

Ndege hiyo yenye chapa AH2017 ilipoteza mawasiliano kwenye muda wa saa saba usiku saa za kimataifa, dakika 50 kabala ya kupaa angani ikitokea katika mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou ikielekea Algiers, nchini Algeria ambako ingelitua saa kumi na dakika kumi saa za kimataifa.

MD-83 de Swiftair, aina ya ndege ya Air Algérie iliyopata ajali ikiwa na abiria 116 alhamisi, Julai 24 mwaka 2014..
MD-83 de Swiftair, aina ya ndege ya Air Algérie iliyopata ajali ikiwa na abiria 116 alhamisi, Julai 24 mwaka 2014.. AFP PHOTO / SAMUEL DUPONT

Awali ikulu ya Paris ilifahamisha kwamba bawa la ndege hiyo limepatikana likiwa limekatika kaskazini mwa Mali, karibu na mpaka na Burkina Faso. Mabaki ya ndege hiyo yenye chapa AH 2017 iko Mali karibu na kijiji cha Boulekessi kwenye umbali wa kilomita zaidi ya hamsini kaskazini ya mpaka na Burkina Faso.

ajali ya ndeg ya Air Algérie yenye chapa AH5017 yazua msisimko.
ajali ya ndeg ya Air Algérie yenye chapa AH5017 yazua msisimko.

Taarifa hiyo inathibitisha taarifa ziliyotolewa alhamisi wiki hii na jeshi la Burkina Faso kwamba mabaki ya ndege hiyo yaliteketea kwa moto na miili ya abiria waliokua ndani ya ndege hiyo imepatikana. Hakuna aliye nusurika katika ajali hiyo. Wachungaji wa mifugo ndio walifahamisha viongozi kuanguka kwa ndege hiyo ya “Air Algerie”, baada ya kuteketea kwa moto ikiwa angani.

“ Ndege hiyo ilichunguzwa vilivyo licha ya kuwa ilikua na matatizo ya kiufundi”. Tangazo la ikulu ya Paris limearifu. Tangazo hilo limeendelea kusema kwamba kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa wametumwa kwenye eneo la tukiyo ili kulinda eneo hilo na kukusanya matokeo ya uchunguzi wa mwanzo.

Mkutano kuhusu ajali hiyo umepangwa kufanyika Ijuma wiki hii, ambamo watahudhuria waziri mkuu wa Ufaransa , Manuel Valls, waziri wa mambo ya nje Laurent Fabius, waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian, waziri wa mambo ya ndani Bernard Cazeneuve na waziri wa uchukuzi Frédéric Cuvillier

“Kwa leo hatuwezi tukathibitisha chanzo cha ajali hiyo”, amesema rais wa Ufaransa, François Hollande. Kwa upande wake waziri wa Ufaransa mwenye dhamana ya mambo ya nje Laurent Fabius, amesma hali yoyote ile inawezekana, kwa hiyo ni kusubiri uchunguzi ukamilike.

Ndege hiyo ya Algeria “Air Algerie” chapa AH 2017 ilipata ajali ikiwa na abiria 116, kutoka mataifa mbalimbali :

Raia 51 wa Ufaransa

27 kutoka Burkina Faso

8 kutoka Libanon

6 kutoka Uhispania

6 kutoka Algeria

4 kutoka Ujerumani

2 kutoka Luxembourg

5 kutoka Canada

1 kutoka Cameroon

1 kutoka Ubelgiji

1 kutoka Misri

1 kutoka Uswisi

1 kutoka Niger

1 Kutoka Mali

1 Kutoka Nigeria

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.