Pata taarifa kuu
ALGERIA-MALI-BURKINA FASO-Usalama wa anga

Algeria : ndege ya Air Algerie yapotea ikiwa na abiria 119

Shirika la ndege la Algeria “Air algerie” limetangaza kwamba limepoteza mawasiliano na ndege yake iliyokua ikitokea katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougo ikielekea Algiers, dakikia 50 baada ya kupaa angani.

A330 ya shirika la usafiri wa ndege la Air Algérie ambayo imepotea ikiwa na abiria 119.
A330 ya shirika la usafiri wa ndege la Air Algérie ambayo imepotea ikiwa na abiria 119. Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo ilikua na abiri 110 kutoka mataifa mbalimbali, na imepoteza mawasiliano ilipokua angani kaskazini mwa Mali, chanzo kiliyo karibu na Air Algerie, ambacho hakikutaka jina lake litajwe, kimesema.

“Idara ya usafiri wa anga nchini Algeria imepoteza mawasiliano na ndege ya shirika la ndege la Air Algerie, ambayo ilikua ikitokea ahamisi wiki hii katika mji wa Ouagagougou ikielekea Algiers, imearifu Air Algerie, ikinukuliwa na shirika la habari la APS.

Air Algerie imefahamisha kwamba Idara ya masuala ya ndege imewasiliana na marubani wa ndege hiyomuda mchache kabla ya kupaa angani.
Zaidi ya wafaransa 50 wanasadikiwa kuwa walikua ndani ya ndege hiyo, ambayo hadi sasa haijulikani ilipo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Air Algerie, shirika hilo la ndege linasafiri mara nne kwa wiki kuelekea Ouagadougou.

“Ndege hiyo haikua mbali na mpaka wa Algeria, wakati walipoomba marubani watuwe aridhini kutokana na hali mbaya ya hewa na kuepuka kugongana na ndege nyingine iliyokua ikitokea Algiers ikielekea Bamako, nchni Mali”, Idara ya usafiri wa anga nchini Algeria imesema katika tangazo iliyotoa leo alhamisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.