Pata taarifa kuu
KENYA-UGAIDI

Polisi nchini Kenya inachunguza taarifa kuwa gaidi "White Widow" mwezi April alikuwa Lamu

Maofisa usalama nchini Kenya wamekanusha taarifa kuwa huenda gaidi wa kike raia wa Uingereza, Samantha Lewthwaite anayefahamika kwa jina la "White Widow" hivi karibuni alisaidiwa na polisi kwenye mji wa Lamu kutembelea kambi ya jeshi la nchi hiyo nchini Somalia. 

Samantha Lewthwaite, gaidi mwanamke raia wa Uingereza anayesakwa na Serikali ya Kenya kwa tuhuma za ugaidi
Samantha Lewthwaite, gaidi mwanamke raia wa Uingereza anayesakwa na Serikali ya Kenya kwa tuhuma za ugaidi REUTERS/Interpol/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa zilizokuwa zimechapishwa kwenye vyombo vya habari nchini humo zimedai kuwamwanamke huyo alipata usafiri wa polisi kwenye visiwa vya lamu na kufika kwenye kambi ya jeshi la Kenya nchini Somalia kabla ya kutoweka.

Hata hivyo kamanda wa polisi kwenye visiwa vya Lamu, Leonard Omollo amekanusha kuhusu taarifa hizi akidai kuwa mwanamke aliyeripotiwa kufika kwenye visiwa hivyo alikuwa ni raia wa Uhispania na alienda kama mtalii na wanatambua kuwa sasa alisharejea nchini mwake.

Kamanda Omollo anasema "Hizi ni tuhuma za ajabu na hazina ukweli wowote, mwanamke huyu alitokea Uhispania na alikuja kama mtalii na tunafahamu kuwa alisharejea kwao". alisema kamanda Omollo.

REUTERS/Joseph Okanga

Msemaji wa jeshi la Kenya. Willy Wasonga alikataa kuzungumzia lolote kuhusiana na taarifa hizi, ingawa taarifa za siri toka ndani ya jeshi la polisi na usalama wa taifa nchini humo zinasema kuwa wameanza kufuatilia taarifa hizi kubaini iwapo ni kweli alikuwa ni raia wa Hispania ama "White Widow" anayesakwa na Serikali ya Kenya kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya kigaidi nchini humo.

Lewthwaite mwenye umri wa miaka 30 hivi sasa amekuwa akihusishwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi duniani la Al-Qaeda pamoja na kundi la Al-Shabab nchini Somalia, makundi ambayo yamekuwa yakitekeleza mashambulizi ya kigaidi kwenye taifa hilo.

Mwanamke huyu ni mjane wa Germaine Lindsay, mtuhumiwa ugaidi anayedaiwa kuwa alihusika na shambulio la kigaidi kwenye terni moja jijini London nchini Uingereza July 7 mwaka 2005 ambapo watu zaidi ya 52 waliuawa.

Lewthwaite ametolewa hati ya kimataifa ya kukamatwa na shirika la polisi wa kimataifa Interpol, hati ambayo ilitolewa kwa maombi ya nchi ya Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.