Pata taarifa kuu
NIGERIA-Usalama

Viongozi wa Nigeria wadaiwa kushindwa kukabiliana na Boko Haram

Siku moja kabla ya mkutano utakaowashirikisha viongozi wa Nigeria, Benin, Chad, Niger Cameroon pamoja na wajumbe wa Marekani na Ulaya mjini Paris nchini Ufaransa, seneta mmoja wa Marekani amebaini kwamba viongozi wa Nigeria hawawajibiki vilivyo kuhusu usalama wa wasichana waliyotekwa nyara.

Maandamano ya kutaka kuachiliwa kwa wanafunzi waliyotekwa nyara na kundi la Boko Haram, yanafanyika kila siku nchini Nigeria, Mei 15 mwaka 2014.
Maandamano ya kutaka kuachiliwa kwa wanafunzi waliyotekwa nyara na kundi la Boko Haram, yanafanyika kila siku nchini Nigeria, Mei 15 mwaka 2014. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya kutowajibika vilivyo kwa viongozi wa Nigeria katika hali ya kuwaokoa wasichana waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram imekua gumzo katika taifa hilo tajiri barani Afrika, hata kwenye balozi mbalimbali za mataifa ya kimagharibi.

Hapo jana alaasiri, siku moja kabla ya taarifa kuhusu ziara ya rais Goodluck Jonathan katika mji wa Chibok leo ijumaa, ambako wasichana hao wanafunzi waliotekwa nyara na wanamgambo wa kundi la Boko Haram, baadhi ya raia mjini Abuja wamekua wakizungumzia suala la usalama kuhusu wasichana hao wakibaini kwamba kuna uzembe upande wa baadhi ya viongozi, huku wengine wakilituhumu jeshi kushindwa kutokomeza kundi la Boko Haram, wakati bajeti ya jeshi iliongezwa mara mbili miaka hii miwili iliyopita.

Jeshi la Nigeria limekua likituhumiwa kushindwa kutekeleza majukumu yake, huku maafisa wa ngazi ya juu jeshini wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya ulaji rushwa wakati usalama wa raia ukiendelea kudorora.

Jenerali Kenneth Minimah (katikati), akitokea kwenye mkutano wa hadhara uliyoshirikisha jeshi pamoja na maseneta wa Nigeria, mjini Abuja, Mei 15 mwaka 2014.
Jenerali Kenneth Minimah (katikati), akitokea kwenye mkutano wa hadhara uliyoshirikisha jeshi pamoja na maseneta wa Nigeria, mjini Abuja, Mei 15 mwaka 2014. REUTERS/Joe Penney

Tuhumu kama hizo zimekua zikitolewa na baadhi ya maseneta wa Marekani , nchi ambayo inachangia kwa kuwatafuta wasichana waliotekwa na kundi la Boko Haram. Marekani imetuma timu ya watu 30 wakiwemo raia wa kawaida, wanajeshi waliobobea katika masuala ya ujasusi na kusamamia usalama pamoja na ndege isiyo na rubani. Wamarekani hao wamenyooshea kidole cha lawama viongozi wa Nigeria wakibaini kwamba hawawajibiki vilivyo kwa kuwatafuta wanafunzi hao waliotekwa nyara, kama alivyoshuhudia muandishi wetu mjini Washington Anne-Marie-Capomaccio.

Mkutano huo utakaofanyika hapo kesho jumamosi katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, ulioombwa na rais wa Nigeria Goodluck Jonathan unalenga kujadili vitendo vya Boko Haram, ambavyo ni tishio kubwa, sio tu nchini Nigeria, bali kwa kanda nzima.

Waandamanaji, katika mji wa Lagos, nchini Nigeria, Mei 14 mwaka 2014, baada ya tangazo la mkutano liliyotolewa na rais wa Ufaransa, François Hollande kuhusu hali ya usalama inayojiri nchi Nigeria, utakaowashirikisha marais wa kikanda, Mei 17 mwaka 2014.
Waandamanaji, katika mji wa Lagos, nchini Nigeria, Mei 14 mwaka 2014, baada ya tangazo la mkutano liliyotolewa na rais wa Ufaransa, François Hollande kuhusu hali ya usalama inayojiri nchi Nigeria, utakaowashirikisha marais wa kikanda, Mei 17 mwaka 2014. REUTERS/Akintunde Akinleye

Mbali na rais wa Nigeria, marais wa Benin, Chad, Niger, Cameroon, waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza, William Hague, naibu waziri wa Marekani wa masula ya siasa, Wendy Sherman, pamoja na muakilishi wa Umoja wa Ulaya watashiriki mkutano huo.

Mkutano huo una lengo pia la kuboresha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Nigeria na Cameroon, ambao umekua umedorora kwa kipindi kirefu kutokana na mzozo wa kimpaka.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.