Pata taarifa kuu
KENYA-Mauaji

Mhubiri wa kiislamu Abubakar Shariff Ahmed auawa Mombasa nchini Kenya

Mhuburi maarufu wa Kislamu mjini Mombasa nchini Kenya Abubakar Shariff Ahmed, alimaarufu kama Makaburi ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasojulikana karibu na Mahakama ya Shanzu mjini Mombasa.

Abubakar Shariff akihojiwa mjini Mombasa oktoba 5 mwaka 2013
Abubakar Shariff akihojiwa mjini Mombasa oktoba 5 mwaka 2013 REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya kifo chake Abubakar, amekua akihofiya usalama wake, na kubaini kwamba maisha yake yako hatarini.

“Maisha yangu yako hatarini, nitauawa siku moja”, Abubakar aliambia AFP, mwezi moja kabla ya kuuawa kwake. Abubakar Shariff Ahmed, muislamu mwenye itikadi kali za kidini, ambaye amekua akichukuliwa na viongozi wa Kenya kama muislamu mwenye itikadi kali za kidini, ameuawa jana jioni mjini Mombasa.

Akituhumiwa kushirikiana na wanamgambo wakiislamu kutoka Somalia nchini Kenya, Abubakar, ambaye alizungumza na AFP februari 20, alijitetea akisema kwamba yeye ni muislamu mwenye itikadi kali za dini, akibaini kwamba huo ndio msimamo wa muislamu bora.

“Uislamu wenye misingi ya itikadi uliundwa dhidi ya wale (...) wanaopinga dini ya Uislamu. Katika Uislamu, hakuna waislamu wenye msimamo wa wastani na waislamu wenye msimamo mkali, sote ni wamoja na dini ni moja ambayo inajikita katika kitabu kitukufu Qor'an, alisema Abubakar kabla ya kifo chake.

Mhubiri huyo wa kiislamu alibaini kwamba Uislamu wa haki ni ule wanofuata wanamgambo wa makundi ya kiislamu kutoka nchini Irak wenye mafungamano na Al-Qaïda, wanamgambo wa kundi la Taliban na wale wa kundi la Al Shabab kutoka Somalia.

Abubakar amekua akituhumiwa kusajili viajana wa kiislamu na kuwasafirsha nchini Somalia kwa minajili ya kujiunga na kundi la Shebab, tuhuma ambazo alikana mara kadhaa.

Hata hivi Umoja wa Mataifa ulimuwekea vikwazo tangu mwaka wa 2012 kutokana na ushirikiano wake wa karibu na viongozi wa kundi la Al Shabab.

Polisi mjini Mombasa wamethibtisha kuuawa kwa Makaburi na wanafanya uchunguzi kubaini waliomuua Mhubiri huyo ambaye amekuwa akituhumiwa na serikali ya Kenya, Umoja wa Mataifa na Marekani kuwasajili vijana na kuwapeleka nchini Somalia kujiunga na kundi la Al Shabab nchini Somalia.

Makaburi ni Mhubiri wa tatu wa Kislamu kuuliwa mjini Mombasa baada ya Abood Rogo aliyeuliwa pia mwaka uliopita kutokana na tuhuma za kuunga mkono mashambuliuzi ya Al Shabab na kutoa mafunzo ya kutatanisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.