Pata taarifa kuu
KENYA-Mashambulizi

Watu sita wauawa katika mashambulizi tofauti mjini Nairobi

Watu sita wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika mtaa wenye wakaazi wengi wa Kisomalia Eastghleigh jijini Nairobi nchini Kenya, baada ya kutokea kwa mashambulizi matatu jana usiku, amesema mkuu wa kitengo kinachokabiliana na majanga nchini Kenya.

Mmoja kati ya waliyojeruhiwa katika mashambulizi yaliyotokea mjini Nairobi afikishwa katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta mjini Nairobi Machi 31, 2014.
Mmoja kati ya waliyojeruhiwa katika mashambulizi yaliyotokea mjini Nairobi afikishwa katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta mjini Nairobi Machi 31, 2014. REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

“Polisi imezidisha ulinzi katika mtaa huo kwa shughuli za uokozi”, amefahamisha mkuu wa polisi katika mji wa Nairobi, Benson Kibue.

“Tunashuku kwamba shambuliyo hilo ni la kigaidi”, mkuu wa polisi wa mji wa Nairobi, Benson Kibue, amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Benson Kibue, amesema watu 25 ndio wamejeruhiwa, na wamesafirishwa katika hospitali mbalimbali.

Mashambulizi hayo matatu yalilenga migahawa na maeneo wanakokusanyika watu wengi katika mtaa wa Eastleigh, mtaa ambao unaitwa mara kwa mara”Mogadiscio ndogo", kutokana na raia waishio katika mtaa huo, ambao wengi wao ni kutoka nchini Somalia.

Polisi imekua ikijaribu kujua ni aina gani vilipuzi viliyotumiwa. Benson Kibue amesema kuwa bomu liliyotengenezwa kienyeji ni moja ya mabomu yaliyotumiwa katika mashambulizi hayo, huku mashahidi wakibaini kwamba gruneti mbili zilitumiwa katika mashambulizi yaliyotokea katika mtaa wa Eastghleigh.

Shambuliyo hilo limetokea, juma moja kabla ya shambuliyo jingine la risase kutokea, ambalo lilisababisha watu sita kuuawa katika mji wa Mombasa, baada ya watu wenye silaha kuwafyatulia risase waumini wa kanisa moja la mtaa wa Likoni.

Viongozi wa Kenya wameonya hivi karibuni kwamba mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wa makundi ya waislamu wenye msimamo mkali yameongezeka, huku wakibaini kwamba hatua kali zimechukuliwa ili kuimarisha usalama katika miji muhimu ya Kenya.

Kenya imekua ikikumbwa na mashambulizi ya watu wenye silahatangu oktoba mwaka 2011, baada tu ya taifa hilo kutuma wanajeshi wake nchini Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.