Pata taarifa kuu

Vyama vya utumishi wa umma kuandamana Ufaransa

Vyama vya utumishi wa umma vimetoa wito wa kugoma Jumanne hii, Oktoba 10 kwa kupinga sera ya kiuchumi ya serikali. Mikusanyiko inatarajiwa kushuhudiwa nchini kote Ufaransa.

Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2007 vyama tisa vya utumishi wa umma vinaandaa mgomo kabambe nchini Ufaransa.
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2007 vyama tisa vya utumishi wa umma vinaandaa mgomo kabambe nchini Ufaransa. FILE PHOTO - Demonstrators attend a national strike and protest
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 2007 vyama tisa vya utumishi wa umma kuandaa mgomo kama huu. Taarifa za mgomo zimewekwa katika hospitali mbalimbali, shule, ofisi za manispa ya miji na hata kwenye ofisi za wozara mbalimbali. Karibu nusu ya walimu wa shule za msingi tawakuwa katika mgomo huo mjini Paris. Maofisa wa polisi wa CFDT na Polisi ya UNSA pia watajiunga na mgomo huu kwa kukataa kile wanachosema mazingira yao ya kazi. Maafisa wa Pole Empoli wataandamana dhidi ya kupunguzwa kwa nafasi za kazi.

Waandamanaji hao watakaua na kauli moja pekee ambayo ni ulinzi wa huduma ya umma. Maosisa wa Polisi wa CFDT wanatazamia kuhamasisha dhidi ya hatua za uchumi za serikali. Katika vituo vyake, kiwango cha kawaida kinachotumika kama msingi wa ongezeko la mshahara na kufutwa kwa nafasi 120,000 katika idara ya utumishi wa umma zilizotajwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Wakati huo huo, muungano wa vyama vya madereva wa magari wa FO na ule wa CGT wameamua kujiunga na maandamano haya kwa kupinga dhidi ya marekebisho ya sheria kuhusu ajira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.