Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Wakazi wa Catalonia wajiandaa kufanya mgomo mkubwa

Sughuli nyingi zinatazamiwa kukwama katika eneo la Catalonia kufuatia mgomo mkubwa ulioitishwa na vyama vya wafanyakazi kulalamikia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ulioshuhudiwa siku ya Jumapili wakati wa kura ya maoni ya kujitawala.

Uso kwa uso kati ya polisi na wapiga kura wa Catalonia, nje ya kituo cha kupigia kura Barcelona, Oktoba 1.
Uso kwa uso kati ya polisi na wapiga kura wa Catalonia, nje ya kituo cha kupigia kura Barcelona, Oktoba 1. REUTERS/Susana Vera
Matangazo ya kibiashara

Wafanyakazi wameapa kutoripoti leo kazini na baadhi ya maduka na sehrmu mbalimbali zitafungwa. Klabu maarufu soka ya Barcelona pia inatarajiwa kugoma, huku vyuo vya umma na makavazi nayo yakitarajiwa kugoma.

Wakati wa zoezi hilo siku ya Jumapili, polisi ilitumia nguvu kwa kujaribu kufunga baadhi ya vituo vya kupigia kura, na wakati huo kulimakabiliano kati ya wanaharakati wapiga kura na askari. Wakati huo mimia ya watu walijeruhiwa.

Kwa upande wa polisi, polisi 3 walijerihiwa, kwa mujibu wa maafisa wa afya katika eneo Catalonia.

Toka awali Uhispania ilipiga marufu kura hiyo na kusem akuwa ni kinyume na katiba ya nchi hiyo. Zaidi ya watu milioni 2.2 walipiga kura.

Mgomo wa leo utavuruga shughuli za usafiri wa umma, shule na zahahati katika eneo nzima la Catalonia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.